loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanawake watakiwa kumuunga mkono Rais Samia

WANAWAKE wametakiwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi zenye tija kwa kuwa uwezo huo wanao.

Kauli hiyo imetolewa na Mteule wa nafasi ya Makamu wa Askofu Mkuu Taifa wa kanisa la Calvary Evangelical Assembly Tanzania, Seth Gidiony wakati wa mahojiano.

Alisema wanawake wanatakiwa kumuunga mkono Rais Samia kwa kufanya kazi kwa bidii na kujiamini kwa kile wanachofanya kwani uwezo huo wanao.

Alisema kila wanapopata nafasi ya kuongoza iwe kwenye

Serikali,jamii,taasisi za kidini wanatakiwa kujiamini kwanza na

kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma  kwa ajili ya maendeleo kama

ilivyoleo hii ambapo Tanzania inaongozwa na mama ambaye ni Rais.

 

Makamu huyo wa askofu Mkuu ambaye pia ni kiongozi wa Jimbo la Dodoma amewataka wanawake kuongeza bidii ya kumwombea Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na wasaidizi wake ili waweze kuongoza Taifa kwa misingi ya kiroho itakayoleta maendeleo kwa Watanzania bila kujali itikadi yoyote.

 

Pia aliwataka vijana hapa nchini kufanya kazi zitakazowaletea

maendeleo ili waweze kuunga mkono juhudi za serikali ambayo imekuwa

ikihimiza kila mtu kujituma kwa ajili ya kujiletea maendeleo ,badala

ya kukaa vijiweni na kuinyoshea vidole serikali.

 

Alisema vijana lazima wafanye kazi zenye tija ili waweze kufikia

malengo yao ambayo yatakayowainua hata kwenye maisha yao na kwenye

mapato na hatimaye kukuza uchumi wa nchi.

 

Aidha aliwataka waumini wa kanisa hilo kutumia muda wao kuiombea

Serikali ili miradi yote ambayo hayati Rais John Magufuli aliyoianzisha

iweze  kukamilishwa kwa wakati.

Mmoja wa waumini wa kanisa hilo Maria Patrick alisema wanawake

wanamuombea Rais Samia ili aweze kutimiza wajibu wake wa kuwatumikia Watanzania.

“Kinamama tuendelee kusimama nae na kumuombea ili aweze kutekeleza

majukumu yake vizuri,” alisema

SERIKALI imezuia ndege zote zinazofanya safari za kwenda ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi