loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vijana 12, 625 waitwa mafunzo ya ufundi

OFISI ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu imetangaza nafasi 12, 625 za mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo 68 vya Veta vya mikoa na wilaya.

Taarifa ya Katibu Mkuu wa ofisi hiyo imewataka vijana raia wa Watanzania wenye umri wa miaka 15 hadi 35 wafike kwenye vyuo husika wachuke fomu za kuomba kujiunga na mafunzo hayo.

Tangazo hilo lilielekeza kuwa, maombi hayo yawasilishwe kuanzia tarehe 19/04/2021 hadi 30/04/2021 yakiambatana na nyaraka ikiwamo nakala ya cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha uraia au kadi ya mpiga kura, barua ya utambulisho kutoka ofisi ya serikali ya mtaa au kijiji anachoishi mwombaji na picha nne za pasipoti zilizoandikwa majina matatu ya mwombaji kwa nyuma.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mafunzo hayo yatakayoanza Mei 17 mwaka huu, yanalenga kuwezesha nguvukazi ya taifa kupata ujuzi na stadi za kazi ili kumudu ushindani katika soko la ajira.

“Serikali itafadhili ada ya mafunzo kwa asilimia 100. Mwanafunzi/mzazi/mlezi atagharamia gharama nyingine zikijumuisha nauli ya kwenda chuoni na kurudi nyumbani. Muombaji anashauriwa kuomba mafunzo haya katika chuo kilicho katika mkoa anaoishi,” ilieleza taarifa hiyo.

Vyuo hivyo vipo kwenye mikoa ya Njombe, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Pwani, Dodoma na Singida.

Taarifa iliongeza kusema kuwa, vijana watakaochaguliwa watapata mafunzo ya ufundi stadi katika sekta za usafirishaji, teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama), madini, kilimo, ujenzi, uzalishaji, ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo, huduma za hoteli na utalii.

“Vijana wenye ulemavu wanasisitizwa kuomba fursa hizi na watapewa kipaumbele katika nafasi za mafunzo haya,” ilisema taarifa hiyo.

Katibu Mkuu ametaja miongoni mwa fani zilizokubaliwa kufundishwa kuwa ni umeme wa majumbani, ufundi seremala, utengenezaji nywele, utengenezaji viyoyozi na majokofu, uungaji na uchomeleaji vyuma, ushonaji nguo, ufundi magari, uashi na utengenezaji wa tovuti.

Alitaja fani nyingine kuwa ni ufundi umeme wa magari, upishi, ufundi bomba, tiba ya urembo, huduma za chakula na vinywaji, huduma za kupokea wageni hotelini, utengenezaji tovuti na matangazo na utunzaji wa kompyuta.

Vijana hayo pia watafundishwa ukarabati wa simu za mkononi, utengenezaji wa vifaa vya aluminiamu, utunzaji wa kompyuta, uandaaji vyumba vya kulala wageni na udobi, utengenezaji na uokaji mikate, na utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki.

Fani nyingine ni upakaji rangi na uandishi wa alama, uwekaji marumaru na terazo, utengenezaji wa viyoyozi vya magari na majumbani, ufundi wa umeme wa jua, utengenezaji wa tovuti na matangazo na ukarabati wa simu za mkononi. 

Waombaji kwa fani ya ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo, ufundi bomba, ujenzi, useremala, uchomeleaji na uunganishaji vyuma, upakaji rangi na maandishi wanapaswa kuwa na elimu ya msingi au zaidi.

Vijana wanaoomba kujifunza fani nyingine zilizobaki wanapaswa kuwa na elimu ya kidato cha nne na kuendelea.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi