loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TRA waenda kwa wafanyabiashara

MAOFISA wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) taifa na wa mkoa wa Kilimanjaro watatembelea wafanyabiashara katika wilaya zote za mkoa huo kutoa ya kutunza kumbukumbu za hesabu na ulipaji kodi kwa mujibu wa sheria.

 Kaimu Meneja Elimu kwa Mlipakodi TRA makao makuu, Rose Maendeka alisema jana kuwa, tayari wameshapita katika mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Singida, Mwanza, Lindi, Mtwara na Mbeya kuelimisha wafanyabiashara kuhusiana na masuala hayo.

 "Tunapita mlango kwa mlango kuzungumza na wafanyabiashara, suala la mfanyabiashara na TRA kama daktari na mgonjwa, tunawaelewesha sheria za kodi, kujua nini changamoto zao, kisha tunakubaliana ulipaji sahihi wa kodi," alisema Maendeka.

 Alisema pia watahimiza matumizi sahihi za mashine za kieletroniki (EFD), nani  wanaostahili kuzitumia, namna wafanyabiashara wanavyoweza kujikadiria kodi na taratibu za kupata vitambulisho vya mjasiriamali.

 Maendeka alisema katika mikoa waliyotembelea walibaini changamoto ya wafanyabiashara kutotunza kumbukumbu za hesabu, kutotoa risiti wakati wa kuuza na kutopata risiti wanaponunua. 

"Kila mfanyabiashara baada ya kusajili TRA anatakiwa kutoa risiti, kuna zile za vitabu ambao mauzo yao ni mil 4 sawa na Sh 13,500 kwa siku, huyo atatoa risiti ya kitabu yenye TIN namba yake na wanaouza Sh 45,600 kwa siku  sawa na Sh milioni 14 kwa mwaka kwa kutumia EFD," alisema.

 Meneja Msaidizi TRA mkoa wa Kilimanjaro upande wa madeni na ufuatiliaji wa walipakodi wanaotumia mashine za EFD, Tirson Kabuje alisema kazi hiyo itafanyika katika maeneo ya Mbuyuni, Kiusa, Kiborlon na baadaye wilayani hadi Aprili 29 mwaka huu.

 Wakati akizungumza na maofisa hao, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Anna Mghwira aliitaka TRA ifute dhana ya kuonekana wanatoza kodi kwa nguvu na wajenge mazingira ya wafanyabishara kulipa kodi kwa hiyari na kwa kuzingatia taratibu na sheria za ulipaji kodi.

 

SERIKALI imezuia ndege zote zinazofanya safari za kwenda ...

foto
Mwandishi: Nakajumo James, Moshi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi