loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kazi za vijana 10,000 zarasimishwa

VIJANA 10,178 wamerasimishiwa kazi zao wakiwemo 28 wenye ulemavu katika Mwaka wa Fedha 2020/21 mpaka kufikia Februari mwaka huu baada ya serikali kuingia mkataba na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) wa kurasimisha ujuzi kwa vijana katika mikoa yote nchini.

Kazi zilizorasimishwa ni katika fani za ufundi wa magari, useremala, uashi, upishi, huduma za vyakula na vinywaji, ufundi umeme, uchomeleaji vyuma, ufundi bomba, uchongaji, vipuri na ushonaji wa nguo.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Patrobas Katambi, alisema hayo bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Latifa Juakali (CCM), aliyetaka kufahamu ni lini vijana wa  Tanzania watapewa stadi mbalimbali za kuwaongezea ujuzi wa maarifa kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa Wananchi Kiuchumi.

Alisema katika Mwaka wa Fedha 2020/21 kufikia Februari, 2021 vijana 10,178 walikuwa wamerasimishwa na kati yao 28, wanaishi na ulemavu.

Hii ilitokana na kutambua umuhimu wa kuwapatia vijana ujuzi wa stadi za kazi na maarifa kama hatua mojawapo ya kuwawezesha vijana kumudu ushindani katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Alisema serikali kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi, imewapa mafunzo vijana 5,538 kwa njia ya uanagenzi katika fani za ufundi stadi katika nyanja mbalimbali kupitia Taasisi ya Don Bosco na vyuo vilivyo chini ya Veta.

Alisema vijana wanaohitimu elimu ya juu wanaendelea kupata mafunzo ya uzoefu kazini na Serikali imeendelea kuwashikiza wahitimu kwa waajiri.

Kwa mujibu wa Katambi, katika Mwaka wa Fedha 2020/21 hadi kufikia Februari, 2021, wahitimu 1,203 wa vyuo vya elimu ya juu na kati, walikuwa wamekamilisha mafunzo ya uzoefu kazini.

Alisema mafunzo hayo ni  kupitia viwanda, taasisi na kampuni mbalimbali za sekta binafsi na umma nchini.

“Wahitimu 2,037 wanaendelea kupata ujuzi na uzoefu katika taasisi mbalimbali binafsi na za umma na kati yao, wahitimu 92 ni watu wenye ulemavu,” alisema.

SERIKALI imezuia ndege zote zinazofanya safari za kwenda ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi