loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maeneo uwekezaji kambi za utalii, loji yabainishwa

MAENEO manne ya uwekezaji yamebainishwa kwa ajili ya ujenzi wa kambi za watalii na loji zenye hadhi za kimataifa katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, katika kuona umuhimu wa maeneo ya uhifadhi katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha  2021/22 pamoja na masuala mengine, imezingatia uimarishaji wa utangazaji wa utalii na kuboresha miundombinu ikiwemo barabara, viwanja vya ndege na maeneo ya malazi kwa wageni ili kuvutia watalii kutembelea maeneo hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja alibainisha hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Makete, Richard Sanga (CCM) aliyetaka kujua mkakati wa serikali wa kutangaza Hifadhi ya Taifa ya Kitulo ili ifahamike kwa watalii wa ndani na nje.

Alisema Hifadhi ya Taifa Kitulo ilianzishwa kwa GN Na. 279 ya Septemba 16 Mwaka 2005, ikiwa na sifa ya kipekee kwa kuwa na jamii mbalimbali za maua na serikali imekuwa ikitangaza hifadhi hiyo na nyingine zilizopo nchini.

“Mikakati  iliyopo kwa sasa ni kuendelea kuzitangaza hifadhi zote za taifa ndani na nje ya nchi ikiwemo Hifadhi ya Taifa Kitulo kwa kutumia mikakati mbalimbali ikiwemo kupitia tovuti na mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook, Twitter  pamoja na kuandaa video na filamu mbalimbali,” alisema.

Alisema wanaimarisha  miundombinu ya barabara ndani ya hifadhi ili kurahisisha kufikika kwa maeneo ya vivutio ndani ya hifadhi, kutangaza hifadhi kupitia chaneli maalum ya utalii ya ‘Tanzania Safari Channel’ na kuandaa safari za mafunzo kwa wanahabari, mawakala na wadau mbalimbali wa utalii ili kuwapa fursa ya kuvielewa vivutio vya utalii na kuvitangaza ndani na nje ya nchi.

Alisema watajenga sehemu za malazi ya bei nafuu kwa ajili ya wageni wa ndani na nje ya nchi; na kuvutia wawekezaji kujenga kambi za watalii/loji zenye hadhi za kimataifa na kwamba, tayari maeneo manne ya uwekezaji yameshabainishwa.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi