loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Washitakiwa wawili wakamilisha taratibu za mazungumzo na DPP

WASHITAKIWA wawili katika kesi ya kukwepa kodi na kuitia hasara ya Sh bilioni 31.48 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya kuuza vinywaji ya Jaruma General Supplies Ltd, Lucas Malya na wenzake watano katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wamekamilisha taratibu za mazungumzo na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Wamekamilisha mazungumzo hayo baada ya kuandika barua ya kukiri na kuomba kumaliza shauri hilo kwa njia ya majadiliano.

Washtakiwa hao Tunsubilege Mateni (Mhasibu) na Nelson Kahangwa (Mkaguzi wa Hesabu) walithibitisha hayo juzi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Issaya, kesi hiyo ilipopelekwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai mahakamani hapo kuwa, shauri hilo lilipelekwa kwa ajili ya kutajwa na alithibitisha kukamilika kwa taratibu zote za kukiri na makubaliano yaliyofikiwa baina ya washtakiwa na DPP ikiwa ni pamoja kufanya malipo waliyokubaliana.

Baada ya kueleza hoja hiyo, Simon aliiomba mahakama iwapangie tarehe nyingine kwa ajili ya kufanya usajili na kumaliza shauri hilo. Hakimu Issaya aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 3, mwaka huu.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Happy Mwamugunda, Prochesi Shayo na Geofrey Urio.

Katika kesi hiyo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 23 ikiwemo kukwepa kodi ya vileo, kuisababishia serikali hasara zaidi ya Sh bilioni 31.48 na kutakatisha kiasi hicho cha fedha.

 

SERIKALI imezuia ndege zote zinazofanya safari za kwenda ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi