loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Soko la Mpakani lapunguza uhalifu

IMEELEZWA kuwa ujenzi wa soko la pamoja la mpakani katika Kijiji cha Mkarazi wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma umechangia kuimarisha usalama na kupunguza matukio ya uhalifu kwa raia na mali zao.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkarazi, Ndize Sebastian alisema hayo katika mahojiano maalumu na HabariLEO na kusema kuwa, kuhamishwa kwa soko hilo kutoka Kijiji cha Mambamba kwenda katika Kijiji cha Mkarazi kumeimarisha hali ya ulinzi na usalama katika eneo hilo.

Awali watu wenye nia ovu walikuwa na nafasi ya kuingia na silaha na kufanya uhalifu kutokana na kutumia fursa ya kuingia kijijini kwa kuvuka vizuizi vya polisi na uhamiaji kwa kigezo cha kufanya biashara huku wakiwa wameficha silaha kwenye bidhaa jambo ambalo kwa sasa limedhibitiwa.

Alisema sasa kumekuwa na ukaguzi mkali kwa watu wanaovuka vizuizi vya polisi na uhamiaji kuingia Kijiji cha Mabamba kutokea Burundi ambapo pia, wananchi wamesimamia kwa karibu jukumu la kudhibiti uhalifu vikiwamo vitendo vya wizi na ujambazi.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mkarazi, Ezekiel Anthony, alisema ujenzi wa soko la Mpakani katika Kijiji cha Mkarazi pia umesaidia kuongeza mauzo kwa wafanyabiashara katika soko hilo.

Mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo, Stella Christopher, alisema Soko la Mkarazi limesaidia kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara sokoni hapo huku kukiwa na ulinzi wa kutosha.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi