loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga yapata kocha mpya wa tatu

 KOCHA mpya wa Yanga, Nasreddine Nabi amewasili nchini jana na kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu, huku akisema anafurahi kuwa sehemu ya benchi la timu hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati.

Amesema atahakikisha kwa uwezo wake timu hiyo inaafanya vizuri maana analifahamu vizuri soka la Afrika.

Nabi ambaye alifukuzwa kazi katika klabu ya El-Merreikh ya Sudan hivi karibuni, anakuwa kocha wa tatu msimu huu kwa klabu ya Yanga, baada ya Zlatko Krmpotic ambaye alifukuzwa mwanzoni mwa msimu na kuajiriwa Cedrick Kaze ambaye naye alifukuzwa baada ya kupata sare nne katika michezo sita na kufungwa na Coastal Union.

Kocha huyo alitua katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Terminal 3, Dar es Salaam jana saa 8:45 mchana akiwa na msaidizi wake na wakala wake Abdul Mussa kutoka kampuni ya Sifeza na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Yanga, Hersi Said.

Akizungumza jana, Nabi alisema Yanga ina historia nzuri na ana imani ya kufanya vizuri na timu hiyo.

“Nahitaji muda kuandaa timu kiufundi na kuweka mipango yangu sawa kwa sababu nimekuja timu ikiwa mwishoni mwa msimu, nina imani kwa ushirikianao mzuri wa uongozi tutafikia malengo yanayotarajiwa na wana- Yanga,” alisema Nabi na kuongeza:

“Nimekuwa nikiifatilia Yanga tangu tumeanza kufanya nao mazungumzo, nina furaha kuwa hapa naamini nitafanya vizuri.” Pia kocha huyo alisema anajivunia kuinoa klabu hiyo kubwa Afrika yenye idadi kubwa ya wachezaji wanaotambulika Afrika na idadi kubwa ya mashabiki.

Baada ya kusaini mkataba jana, Nabi ataanza kazi mara moja akichukua mikoba ya Cedric Kaze aliyetimuliwa hivi karibuni.

KOCHA wa Simba, Didier Gomes na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi