loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sheria zinazosimamia AZAKI zajadiliwa

WADAU mbalimbali kutoka asasi za kiraia wamekutana kujadili matakwa ya sheria na miongozo inayosimamia na kuratibu sekta za Asasi za Kiraia nchini Tanzania baada ya sheria hizo kufanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Baadhi ya sheria hizo ni kuweka wazi mikataba yao ya kifedha za ufadhili kati yao na wawezeshaji pamoja na kupeleka taarifa zao za fedha za kila robo mwaka.

Meneja Idara ya Kujenga Uwezo kutoka  Foundation for Civil Society (FCS), Edna Chilimo alisema asasi za kiraia 300 zilikutanishwa ambapo mada mbalimbali zilitolewa kwa lengo la kutoa elimu na uelewa mpana kwa asasa hizo kuhusu maboresho ya sheria hizo.

Alisema mada hizo zilitolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Usajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs), Usajili wa Jumuiya za Kijamii na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA).

Alikiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika  uelewa na tafsiri ya sheria mbalimbali kwani wapo waliokuwa hawazielewi, wengine walikuwa na tafsiri potofu na wengine kuhamaki.

“Kwa kuona tatizo hilo FCS kama Mwezeshaji  tukashirikiana na wadau wengine ambao ni Mashirika ya kimtandao  NaCoNGO, TANGO na  Equality For Growthi (RfG) kutengeneza Programu ya kuziwezesha asasi za kiraia kuelewa sheria hizo vizuri na kupata tafsiri sahihi.

“ Ili mwisho wa siku waweze kuzifuata na kuzifanyia kazi waweze kutekeleza miradi yao kwa weledi wakiwafikia wananchi na kuhakikisha wanafuata sheria hizo,” alisema.

Kwa upande mwingine alisema program hiyo pia inalenga  kutoa msaada kwa yale mashirika yaliyokuwa yanahitaji msaada wa kitaalamu  ili yaweze kuelewa zaidi ili kila mmoja aweze kufikia malengo.

“Programu hii tunaifanya kwa karibu na watu wa Serikali kwa kuwa wao ndio wasimamizi wa hizo sheria hivyo tumefanya kazi na Ofisi ya msajili wa NGOs, Ofisi ya Msajili wa Jumuiya na RITA,” alisema.

Alisema wataalamu hao kutoka serikalini walifafanua mambo mbalimbali yanayohusu AZAKI kuanzia kusajiliwa, namna ya kufuata Sheria na Sheria zenyewe jambo litakalosaidia  wadau kuweza kufahamu maeneo tofauti ya kufanya kazi kwa kufuata Sheria

Alisema FCS inaendelea kutoa uelewa juu ya sheria hizo kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali kutoka katika taasisi za serikali ili kuendelea kukuza uelewa mpana zaidi.

FCS kwa kushirikiana na  Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Serikali (TANGO)  pamoja na EfG yamekutanisha wadau mbalimbali kutoka  asasi za kiraia kwa lengo la  kujadili   matakwa ya sheria na miongozo.

SERIKALI imezuia ndege zote zinazofanya safari za kwenda ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi