loader
Dstv Habarileo  Mobile
Aliyemuua Floyd akutwa na hatia

Aliyemuua Floyd akutwa na hatia

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani aliyekuwa Afisa wa Polisi wa Jimbo la Minneapolis, Derek Chauvin kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd kilichotokea Mei 25, 2020.

Licha ya kukataa mauaji hayo mara tatu, Chauvin amekutwa na hatia ya kufanya mauaji na kuamuriwa kurudishwa mahabusu hadi pale hukumu yake itakaposomwa. Uamuzi huo uliwafurahishwa baadhi ya wanaharakani na raia wa nchi hiyo.

Wakili wa familia ya Floyd, Ben Crump alisema ni hatua ya "muhimu hatika historia" ya Marekani."haki iliyotafutwa kwa uchungu hatimaye imepatikana, aliandika kupitia ukurasa wake wa  twitter . Rais Joe Biden na Makamu wake Kamala Harris waliipigia simu familia ya Floyd mara baada ya uamuzi huo, Biden alisikika akisema "hatimaye haki imetendeka".

"Tutaongeza juhudi kuhakikisha mengine yanafikiwa. Hii itakuwa hatua ya kwanza muhimu ya kukabiliana na ubaguzi wa rangi uliokithiri katika mifumo yetu," alisema Rais Biden.

Wakati huo huo, Kamala Harris aliwahimiza wabunge kupitisha muswada wa George Floyd unaolenga kurekebisha idara ya polisi nchini Marekani . "Muswada huu ni sehemu ya urithi wa George Floyd. Kazi hii ni ya muda mrefu," alisema Harris.

George Floyd (46) aliuawa baada ya Polisi huyo kumkandamiza shingoni kwa kutumia goti baada ya kuamuriwa kutoka kwenye gari lake kwa ajili ya kufungwa pingu baada ya kusemekana kuwa alinunua sigara kwa kutumia sarafu bandia ya Dola 20 ya Kimarekani.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/b479f7f90f0db02d9c88e79723260237.jpg

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameweka jiwe la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi