loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wananchi Mtwara wadaiwa kukata nyaya za umeme kisha kuvulia pweza

SHIRIKA la Umeme mkoani Mtwara TANESCO), limewataka viongozi wa kata na vijiji vilivyopo kando kando ya bahari kuhakikisha wananchi wa maeneo yao wanaacha tabia ya kuharibu miundombinu ya umeme na kusababisha kukatika kwa nishati hiyo mara kwa mara.

Ofisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mtwara, Jumanne Mkunguu alitoa wito huo jana na kusema kuwa miongoni mwa sababu za kukatikatika umeme katika vijiji hivyo ni kukatwa kwa nyaya za kushikia nguzo za umeme na kutumiwa katika kuvulia samaki aina ya pweza.

 “Taarifa ambazo tunazo zinasema kwamba wananchi wa maeneo ya vijiji na kata zinazopakana na bahari wanakata nyaya za kushikia nguzo kwa ajili ya kukata vyuma vya kuvulia samaki aina ya pweza,” amesema na kutoa wito kwa viongozi wa maeneo hayo kuhakikisha wananchi hao wanaacha mara moja kuharibu miundombinu ya umeme na kusababisha kukakatika mara kwa mara.

Mkunguu amesema tatizo la kukatikakatika umeme ni kubwa katika vijiji vya kandokando ya bahari. Ametaja baadhi ya maeneo yenye tatizo kubwa la kukatikakati umeme kuwa ni MsangaMkuu, Msimbati na Naumbu

 “Kwa mfano tulienda Kijiji cha Mgao ambao wamekosa umeme kwa siku nne na moja ya sababu kubwa inayotajwa ni kukatwa kwa nyaya za umeme na kusababisha nguzo kuanguka. Niwasihi viongozi wahakikishe wananhci wanalinda miundombinu ya umeme kwa sababu shirika la umeme ni shirika la umma ambapo na wao ni wahusika,” alisema.

Wakizungumza wakati wa ziara hiyo baadhi ya viongozi wa kata walikiri kuwepo kwa tatizo la kukatikakatika nyaya za umeme huku wakiitaka kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujua umuhimu wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao.

Mtendaji wa Kata ya Naumbu Kaiza Mnete alikiri kuwepo kwa changamoto ya kukatwakatwa kwa nyaya za kushikia nguzo za umeme katika vijiji vya kata hiyo huku akisema tatizo ni wananchi kukosa elimu kuhusu umuhimu wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao.

Mmoja wa wavuvi walikana kutumia nyaya za umeme katika kuvulia samaki huku wakiahidi kutoa ushirikiano kwa shirika hilo katika kuwabaini wanaotumia nyaya hizo za umeme kuvulia samaki.

“Mimi ninachoona ni kushirikiana na Tanesco kwa ajili ya kubain wanaohusika kama ni kweli basi wale wanaohusika wachukulie hatua, ila kwa mimi situmii hizo nyaya katika uvuvi wangu,” amesema Ally Mohammed mvuvi wa kata ya Mgao Halmashauri ya Mtwara.

SERIKALI imezuia ndege zote zinazofanya safari za kwenda ...

foto
Mwandishi: Anne Robi, Mtwara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi