loader
Dstv Habarileo  Mobile
Klopp:  Hatustahili kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya

Klopp: Hatustahili kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kikosi chake hakijapambana vya kutosha na hakistahili kuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya sare ya bao 1-1 na Newcastle United kwenye uwanja wa Anfield juzi.

Kikosi cha Klopp kililenga mashuti 22 golini katika mechi hiyo, lakini kilipata bao moja tu lililofungwa na Mohamed Salah katika dakika tatu za mwanzo wa kipindi cha kwanza.

Joe Willock alifunga bao la kusawazisha katika dakika tano za majeruhi na kutoa sare kwa kikosi cha Steve Bruce na kuweka shakani matumaini ya Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa.

“Sidhani kama unaweza kutengeneza nafasi zaidi, tulikuwa na nafasi nzuri lakini tulishindwa kumaliza mechi, hatukucheza vya kutosha,” alisema Klopp baada ya mechi.

“Kwa ujumla hatupambana vya kutosha, tulikuwa na asilimia 70, tulipaswa kuwa na 80, tulitengeneza nafasi nyingi, hivyo tulipaswa kutengeneza nafasi lakini hatukufanya hivyo ni kama tumefungwa hivi.”

“Sijaona kama leo (juzi) tunastahili kucheza Ligi ya Mabingwa mwakani. Lakini tutaona tunachoweza kufanya, siku chache zijazo tutacheza na Manchester United, mechi itakayokuwa ngumu pia, lakini tunajifunza au tusicheze Ligi ya Mabingwa, ukweli ni huo.”

Liverpool ipo nafasi ya sita pointi moja nyuma ya Chelsea na West Ham United. Kikosi cha Klopp kina mechi kadhaa muhimu kama kinataka kufuzu kwenye nne bora ikiwemo dhidi ya United Mei 2.

Newcastle ilipata bao kutoka kwa Callum Wilson lakini lilikataliwa na Klopp alisema walikuwa na bahati kwa maamuzi hayo kwani yaliwasaidia.

“Tunatakiwa kuendelea kupambana, kuendelea kucheza, lakini tuliwaweka hai na walistahili bao kwa sababu walifunga kabla yetu,” alisema

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/addee250d416cf2acbd0766ad9e0760e.jpg

OLE Gunnar Solskjaer amesema, kuwasili kwa ...

foto
Mwandishi: Liverpool, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi