loader
Azam yafufua matumaini ya ubingwa

Azam yafufua matumaini ya ubingwa

BAADA ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya waajiri wake wa zamani Yanga, Kocha  Mkuu wa timu ya Azam FC, George Lwandamina amesema bado yupo katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya kuzidiwa pointi nne na vinara Simba.

Katika mechi ya Azam na Yanga iliyochezwa juzi, Wanalambalamba hao walifunga bao hilo katika dakika ya 86 kupitia kwa kinara wa ufungaji Ligi Kuu, Prince Dube, akitumia vema mpira mrefu uliopigwa na nahodha Agrey Morris na kufunga bao hilo pekee katika mchezo huo.

Ushindi huo umeiacha Azam FC katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa wamejikusanyia pointi 54 nyuma ya Yanga inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 57.

Akizungumza na gazeti hili baada ya mchezo huo,  Lwandamina alisema  amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake kwa kutimiza kazi waliyopewa na sasa wanarejea tena katika mbio za kulisaka taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

 “Ulikuwa mchezo mgumu wenye presha kubwa kwetu, nashukuru tumepata matokeo mbele ya timu bora, tulikuwa vizuri tulitengeneza nafasi nyingi kama tungeongeza umakini tungepata ushindi mkubwa zaidi ya huu,” alisema Lwandamina.

Naye Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi alisema mchezo ulikuwa mzuri wameadhibiwa kutokana na makosa waliyofanya, lakini hiyo haiwezi kuwakatisha tamaa katika mipango yao ya michezo ijayo.

“Nawapongeza wapinzani wetu walikuwa bora ndio maana wamepata ushindi, tunarudi kujipanga kurekebisha tulipokosea ili tusirudie makosa katika michezo inayofuata,” alisema Nabi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/28d806c534782d64ace3f9d6159ecd9e.jpeg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi