loader
Serikali: Tutaendeleza ujenzi barabara kadri ya upatikanaji fedha 

Serikali: Tutaendeleza ujenzi barabara kadri ya upatikanaji fedha 

SERIKALI itaendelea na ujenzi na matengenezo ya barabara nchini ikiwemo Moshi Vijijini kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.

Akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi, lililohoji ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Rais wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015 ya Ujenzi wa Kiwango cha lami barabara yenye kilomita 13 kuanzia Rau Madukani-Mamboleo-Shimbwe Juu katika Jimbo la Moshi Vijijini.

Akazungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Naibu Waziri wa wizara hiyo, David Silinde alisema kuwa Serikali imeendelea kutekeleza ahadi zilizotolewa na Waheshimiwa Marais walizozitoa katika Awamu zote kwa awamu. 

Alisema, “ Serikali itaendelea na ujenzi na matengenezo ya barabara nchini ikiwemo Moshi Vijijini kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.

“Katika mwaka wa fedha 2018/19 na 2019/20 Serikali imejenga kipande cha barabara chenye urefu wa mita 288 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Shilingi milioni 190 katika barabara ya Rau Madukani-Mamboleo-Shimbwe Juu,” alisema Silinde 

Aidha, katika mwaka wa fedha 2018/19, barabara hii ilifanyiwa matengenezo ya muda maalum yenye urefu wa kilometa 9 kwa kiwango cha changarawe ambayo iligharimu Sh milioni 148.85. Vilevile katika mwaka wa fedha 2021/22 barabara hii imetengewa bajeti ya Sh milioni 10 kwa ajili ya matengenezo ya sehemu korofi yenye urefu wa kilometa mbili.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7d40e72801005d9870cf769a0b86e198.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck, Dodoma 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi