loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wenger aunga mkono tajiri mpya Arsenal 

KOCHA wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amedokeza kuwa yuko tayari kuungana na bilionea mwanzilishi wa Spotify, Daniel Ek pamoja na wachezaji wake watatu wa zamani, katika zabuni ya pandi bilioni 1.8 kuinunua klabu hiyo kutoka kwa Stan Kroenke.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Star, Ek mwenye utajiri unaokadiriwa kuwa Pauni bilioni 3.5 ana mpango madhubuti wa kuinunua Arsenal kwa kushirikiana kwa pamoja na magwiji wa klabu hiyo, Thierry Henry, Patrick Vieira na Dennis Bergkamp. 

Aidha, mazungumzo juu ya uwezekano wa kuichukua klabu hiyo yakiendelea, Wenger amesema yuko tayari kusaidia timu yake ya zamani "kwa njia yoyote".

Hata hivyo ripoti hiyo imeeleza kuwa wamiliki wa sasa wametoa taarifa wakisisitiza hawana mpango wa kuiuza klabu hivi karibuni.

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: LONDON, England 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi