loader
Dstv Habarileo  Mobile
SAFARI YA RAIS SAMIA CCM   

SAFARI YA RAIS SAMIA CCM  

RAIS Samia Suluhu Hassan alikuwa Kada wa CCM tangu utotoni mwake lakini alikuwa mwanachama rasmi wa CCM mnamo 1987, akiwa na umri wa miaka 27, ikiwa ni miaka 10 tangu alipoajiriwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kutokana na Elimu yake na uzoefu wake kama mwanachama wa mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali pamoja na uzoefu wake katika kamati tofauti, amekuwa mjumbe wa Kamati za Kuandaa Ilani za Uchaguzi za CCM kuanzia mwaka 2005 mpaka 2015. Ilani alizoshiriki kuziandaa zimefanikisha ushindi wa CCM sambamba na kuiletea Tanzania maendeleo makubwa.

 Kuanzia mwaka 2012 mpaka sasa, Samia amekuwa Mjumbe wa Halamashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

 Mnamo mwaka 2015 na 2020, Samia alikuwa mgombea mwenza wa Hayati Dk Magufuli  katika chaguzi za Urais.

 Sifa kubwa ya Samia ni kwamba amekuwa mtu ambaye hana makuu na mnyenyekevu tangu 1977 alipoingia kwenye utumishi wa umma, na tangu 1987 alipojiunga rasmi na shughuli za kiutendaji.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/73ce9a16fe2e29467a87ad02db3ab7a4.jpeg

HIVI karibuni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma  

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi