loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kiki ni muendelezo wa anguko la Bongo Flava

Kiki ni muendelezo wa anguko la Bongo Flava

KADIRI siku zinavyozidi kwenda muziki wa Bongo Flava umeendelea kushuka thamani yake katika jamii na kusababisha mashabiki wazidi kupungua kuupa sapoti muziki huo.

Muziki huu ambao kwa muda mrefu uliwathaminisha sana wasanii kama vile Ambwene Yesaya ‘Ay’, Seleman Msindi ‘Afande Sele’, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, Hamis Mwinjuma ‘Mwana Fa’, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambao wengine kupitia heshima ile waliyopata katika muziki wamepata nafasi ya kuingia bungeni.

Lakini tofauti na sasa hivi, wasanii wanaochipukia katika kiwanda cha Bongo Flava wamekuwa hawana thamani tena mbele ya jamii kutokana na kukosa ubunifu

na kuigana na kufanya waonekane wahuni kutokana na jinsi walivyoamua kuufanya muziki huo.

Muziki huo umevamiwa na wasanii wengi wasiokuwa na maadili, ambao kwa kiasi kikubwa wamechangia kuuporomosha muziki huu, ambao ulikuwa ukipendwa na vijana hadi wazee kutokana na mtindo wake na mashairi.

Kutokana na kiki hizo imekuwa jambo la kawaida kwa wasanii kushinda Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) wakihojiwa wengine wakipewa onyo na wakati mwingine kufungiwa pamoja na kupigwa faini kutokana na kufanya mambo yasiyofaa.

Hivi sasa muziki huu umekumbwa na vitendo vingi visivyopendeza ‘kiki’ vinavyofanywa na wasanii pindi wanapotaka kutoa nyimbo zao ili kuwafanya wafuatiliwe zaidi na watu mbalimbali nje na ndani ya nchi.

Wasanii wameamua

kuchagua staili hii ya maisha, ambayo haipendezi kabisa lakini ajabu ilioje kila msanii hasa chipukizi wamekuwa wakitamani kupitia njia hii wakiamini kuwa ni rahisi kufahamika zaidi mbele ya mashabiki wa muziki huo.

Hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na watangulizi wao ambao wamekosa ubunifu na kuwekeza muda mwingi katika kiki, ambazo haziwasaidii wao pamoja na muziki wa Bongo Flava ambao umekuwa ukifuatiliwa zaidi hivi sasa.

Maisha ya kiki yamesababisha wapoteze mvuto mbele ya jamii ambayo zamani iliamini kuwa wasanii ni kioo wakiangaliwa kama waburudishaji lakini pia waelimishaji hasa katika yale mambo makubwa yaliyokuwa mjadala hapa nchini.

Rejea wimbo wa starehe ulioimbwa na wasanii Feruz Mrisho ‘Feruuz’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’, ambapo wimbo wao ulikuwa ukitumika katika matamasha mbalimbali ya kuhusu mad-

hara ya ugonjwa wa ukimwi.

Wasanii hawa walifanya kazi hiyo miaka ile bila kiki, lakini kile walichokifanya kimekuwa alama katika muziki wa Bongo Flava ambao sasa umepoteza dira.

Hii inachangiwa na kukosekana kwa ubunifu kutoka kwa wasanii ambao nyimbo zao nyingi zimekosa maadili mbele ya jamii ambayo ndio walaji wakuu wa kazi zao.

Naamini iwapo kama wasanii wataamua kuwekeza muda wao na kuongeza ubunifu katika kufanya kazi nzuri na kuachana na kiki muziki wa Bongo Flava utarudi katika kilele cha ubora wake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo ilijikusanyia mashabiki wengi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a3ddac388bf40c65a2c8eb3f04afd4d2.png

LIGI Kuu ya Tanzania inaelekea ukingoni ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi