loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SERIKALI YARIDHIA MIKATABA 37 YA KAZI

Serikali imekwisharidhia mikataba ipatayo 37 ya Shirika la Kazi Duniani, ambapo miongoni mwa mikataba hiyo inahusu masuala ya uhuru wa kujumuika, ulinzi, wajibu na haki za wafanyakazi, pia majadiliano ya pamoja kati ya wajiri, serikali na wafanyakazi katika dhana ya utatu.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akitoa hotuba mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi kitaifa jijini Mwanza.

Aidha, amesema mikataba hiyo imepelekea taifa kutunga sheria mbalimbali ili kuleta mahusiano mema katika sehemu za kazi, lakini pia kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi na waajiri na kuhakikisha kwamba serikali inaweka mifumo mizuri ya hifadhi ya jamii.

Pia ameeleza kuwa, ili kuweza kutekeleza sheria na mikataba hiyo, serikali imeruhusu masuala ya uhuru wa kujumuika, majadiliano ya pamoja na kuwezesha maeneo ya kazi na wafanyakazi wenyewe kuanzisha vyama vya wafanyakazi.

Amesema kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, serikali imekwisha sajili vyama 33 vya wafanyakazi na viwili vya waajiri, mashirikisho mawili ya wafanyakazi na mawili ya waajiri na kuwa wajibu wa vyama hivyo ni pamoja na kulinda na kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi na waajiri mahala pa kazi. 

Ameongeza kuwa serikali inavitegemea vyama vya wafanyakazi viwe daraja la mahusiano mema na yenye tija kati ya wajiri na wafanyakazi. 

WATU wa kada tofauti wameelezea panga pangua ya ...

foto
Mwandishi: Isdory Kitunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi