loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Samia: Sitaongeza mishahara mwaka huu

RAIS  Samia Suluhu amesema kutokana na mdondoko wa kiuchumi hawezi kuongeza mshahara mwaka huu.

Rais Samia ameyasema hayo leo mjini Mwanza ambako alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi, Kitaifa yamefanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo.

Rais Samia alisema, “Ndungu zangu mimi ni mama, na mama ni mlezi, lakini kuna msemo wa Kiswahili unasema, maskini hapendi mwanae, maana yake hata kama unataka mwanao apendeze lakini ikiwa huna uwezo wa kumfanya mwanao apendeze utaonekana humpendi.

“Kama nilivyosema awali dai la msingi, mishahara haijapandishwa muda mrefu, hata hivyo kutokana na mlipuko wa janga la corona duniani, hali ya uchumi imeporomoka...

"... Tanzania pia imeathirika, uchumi umeporomoka kutoka wastani wa asilimia 6.9 hadi asilimia 4.7 mwaka huu, hii ina maana uwezo wetu kiuchumi umepungua, imekuwa ni vigumu kwangu kuongeza mishahara, kwanza na ndio nimeingia sijakaa vizuri,” alisema Rais Samia.

Hata hivyo alisema ili kuwapunguzia watu ukali wa maisha, anatarajia kufuta tozo mbali mbali ikiwemo kupunguza makato ya mishahara.

"Serikali imesikia ombi la wafanyakazi la kutaka kupunguziwa kodi inayotozwa kwenye mshahara ya PAYE na pia kutokatwa kodi katika stahiki nyingine, Serikali imeliona jambo hili na tumeamua kupunguza asilimia moja ya makato ya PAYE itatoka asilimia 9 hadi asilimia 8" .

“Pia Serikali imejipanga kupunguza viwango vya kodi vya mishahara kwa watumishi na kuendeleza jitihada za kudhibiti mfumuko wa bei, hivyo nimatumaini yangu itapunguza ukali wa maisha, mwakani Mungu akijalia siku kama ya leo tutapandisha mishahara," alisema 

Awali Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Said Wamba akisoma risala ya wafanyakazi liliomba mishahara ya watumishi wa umma iongezwe na kima cha  chini kiwe Shilingi 970,000, 

 

“Mishahara haijaongezwa kwa miaka nane kwa sekta binafsi na sita kwa watumishi wa umma, hali hii imesababisha kupunguza hali na mori wa kazi hivyo kupunguza ufanisi wa kazi na gharama za maisha zimeendelea kupanda.”

 

Alisema, kima cha chini kwa sasa kwa wafanyakazi wa majumbani ni Sh 40,000 hadi Sh 60,000 huku wa viwandani ikiwa ni Sh100,000. Wakati kwa watumishi wa umma ni Sh 300,000 ambazo zimetangazwa mwaka 2015.

 

Wamba alisema, Tucta ilifanya tatifiti mbili ikiwemo 2006 ambapo ulibaini kwamba kima cha chini cha mshahara kinachotosheleza ni Sh.315,000.

 

“2014 tulifanya utafiti mwingine na kubaini Sh 720,000 kwa wakati huo kingemuwezesha mfanyakazi kumudu kazi yake licha ya kutofikiwa kiwango hicho, mpaka sasa gharama za maisha zimeendelea kupanda na kuumiza watu wa sekta zote na kufanya wafanyakazi na familia kuishi chini ya mstari wa umasikini,” alisema .

 

Kaimu katibu Mkuu huyo alisema Tuta inapendekeza kiwango cha chini cha mshahara kiwe Sh 970,000 ambacho kinakidhi hali halisi ya maisha ya sasa

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetuma salamu ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi