loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tume yatakiwa kutenda haki kupandisha madaraja walimu

KATIBU  wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Paulina Nkwama  amewataka watumishi wa Tume hiyo kuhakikisha wanazingatia muongozo uliotolewa na Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kushughulikia upandishaji wa madaraja ya walimu ili kuhakikisha haki inatendeka.

Aliyasema hayo juzi wakati wa ziara yake wilayani Ukerewe .

Akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Ajira, Maadili na Maendeleo ya Walimu, Christina Hape na Mkurugenzi Msaidizi Maadili na Nidhamu, Robert Lwikolela, Nkwama alisema kuwa TSC imedhamiria kuondoa kero za walimu na kuwataka wazingatie taratibu zilizowekwa na kujiepusha na masuala ya upendeleo wakati wa kutoa huduma kwa walimu.

Nkwama aliwataka watumishi wa TSC wilayani hapo kufanya ziara mashuleni kwa lengo la kutoa elimu kwa walimu juu ya msuala ya ajira, maadili na maendeleo yao ili walimu waweze kuwa na uelewa mpana juu ya wajibu na haki zao katika utumishi wa umma.

Aliongeza kuwa kuwafikia walimu mara kwa mara na kuwapa elimu kunasaidia walimu kujiepusha na makosa ya kinidhamu ambayo baadhi yao wanayafanya kwa kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya sheria kanuni na taratibu za utumishi wa walimu.

Alisisitiza kuwa TSC haina vyombo vya usafiri vya kutosha katika ofisi za wilaya, watumishi wa wilayani wanapaswa kuwa na ushirikiano wa karibu na ofisi za Halmashauri, kufanya kazi kama timu moja na kufanya ziara pamoja na watumishi wa sekta ya elimu wa halmashauri badala ya kukaa na kulalamika kuwa wanashindwa kufanya kazi kwa kuwa hawana vyombo vyo usafiri.

WATU wa kada tofauti wameelezea panga pangua ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi