loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

...Aleta neema bima ya afya, wadaiwa HESLB

RAIS Samia Suluhu Hassan amefuta asilimia sita zilizokuwa zikitozwa kwa wadaiwa wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) badala yake, zitabaki asilimia 15 zinazokatwa kwenye mshahara wa wanufaika.

Vile vile ameongeza umri wa utegemezi kwa bima ya afya kutoka miaka 18 hadi miaka 21 na kusema serikali inakusudia uamuzi huo kuujumuisha kwenye sheria ya bima. Akihutubia sherehe za Mei Mosi jana jijini Mwanza, alisema mtoto wa umri wa miaka 18 bado ni tegemezi.

Mambo hayo na mengine aliyoyatolea utatuzi jana, sehemu kubwa yaliwasilishwa kwake na wafanyakazi kupitia Shirikisho lao (TUCTA).

“Tumeamua kubakiza asilimia 15 inayokatwa kwenye mshahara na kufuta asilimia sita tulizokuwa tukitoza zaidi. Lakini nisisitize deni hili waliokopa waendelee kulipa,” alisema na kuagiza HESLB kuondoa hiyo asilimia.

Hata hivyo aliipongeza bodi kwa kufanya kazi nzuri ya kukusanya madeni na kubainisha kwamba kasi imeongezeka na kuwezesha kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi hao wa elimu ya juu.

“Nawasihi wanufaika kuendelea kulipa,” alisisitiza na kubainisha kwamba, awali alipofika uwanjani hapo alidhamiria kusema ataliangalia suala hilo lakini akaona ni vyema alitolee msimamo papo hapo kwa kufuta kiwango hicho.

Watumishi la 7

Rais Samia alitoa mwongozo kwa waajiri kuwalipa watumishi wenye elimu ya Darasa la Saba waliositishwa utumishi wao huku akiwataka kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.

“Wapo ambao hawajalipwa kutokana na kisingizio kwamba serikali haikutoa muongozi mahususi wa kulipa madai hayo. Muongozi ni huu,” alisema na kuitaka Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kusimamia suala hilo kila mwenye haki aipate.

Ajira za kigeni

Aliagiza mamlaka zinazohusika na usimamizi wa ajira za kigeni, hususani wizara kusimamia suala hili kwa mujibu wa sheria na kuzingatia maslahi mapana ya taifa.

Kuhusu uundaji Mabaraza ya Wafanyakazi, Rais Samia alisema zipo taasisi 40 ambazo hazijay aunda ambazo ameziamuru kufanya haraka kutekeleza hilo. Alishauri pia sekta binafsi ambazo hailazimishwi na sheria, pia kuwa na mabaraza hayo kwa kuwa yana faida kubwa.

Aliwakumbusha waajiri kwamba suala la kuanzisha vyama vya wafanyakazi na uhuru wake si la hisani bali ni la kisheria. “Waajiri watoe fursa kwa wafanyakazi.

Na viongozi wahakikishe haviwi chanzo cha migogoro sehemu za kazi,” alisema na kuagiza viongozi wa wafanyakazi kuwasilisha taarifa za unyanyasaji na udhalilishaji katika maeneo yao ya kazi.

Vibali ajira za wageni

Rais alisema vibali kwa raia kisiwe kikwazo kwenye shughuli za wawekezaji hivyo vitolewe kwa kuzingatia sheria lakini pia maslahi mapana ya taifa.

Aliagiza Wizara ya Kazi,Ajira na Maendeleo ya Vijana kuangalia vizuri suala la mawakala wa ajira ambao alisema wamegeuka waajiriwa wenyewe. “Naomba watupiwe jicho wafanye kazi bila kusababisha migogoro maeneo ya kazi,” alisema.

Wakati huo huo Rais Samia aliupongeza Mkoa wa Mwanza kwa kukipa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 na kuwaahidi kukamilisha miradi mbali mbali ya kimkakati iliyopo mkoani humo.

Awali, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo alisema ni wajibu wa chama kushiriki sherehe hizo pia kuhakikisha zinajenga tabasamu kwa wafanyakazi. Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwataka wafanyakazi kuwa waaminifu katika sehemu zao za kazi.

WATU wa kada tofauti wameelezea panga pangua ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi