loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DK MWINYI AAHIDI WAFANYAKAZI MASLAHI MAZURI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amesema serikali ina malengo mazuri ya kuzitatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi ili waweze kutekeleza vyema majukumu yao.

Alisema hayo jana katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil, Kikwajuni wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa umma wa sekta mbalimbali wakiwemo wa serikali na binafsi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.

Dk Mwinyi alisema serikali inathamini na kutambua mchango na umuhimu wa wafanyakazi katika kuleta maendeleo, utekelezaji mzuri na kuhakikisha kuwa iko wazi kwa ajili ya kuwatumikia wafanyakazi wake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramadhani Soraga alisema wizara yake ina ushirikiano mkubwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwani imesaidia kutoa mafunzo kwa vijana wapatao 200 na kujipatia ajira. 

Alisema janga la corona bado linaathiri wafanyakazi na kukwamisha maendeleo na pia kuathiri uchumi wa nchi, hivyo wizara itaendelea kushirikiana na vyama shirikisho kuona hali inaimarika katika kila sekta na utendaji wa kazi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Mwatum Khamis Othmani akisoma risala alisema bado kuna baadhi ya watendaji wenye nyadhifa za juu hujifanyia marekebisho katika mishahara yao na kuwadhalilisha wafanyakazi wa chini.

Siku Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani hufanyika kila na kauli mbiu ya mwaka huu kwa Zanzibar ni “Uwajibikaji na haki ndio msingi wa maendeleo Zanzibar.”

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetuma salamu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi