loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasomi, wanasiasa wapongeza mabadiliko CCM

WASOMI, wanasiasa na wananchi wamesema ushindi wa kishindo aliopata Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan unatokana na imani ya watu iliyojengwa kwa kiongozi huyo.

Maoni hayo yalitolewa jana kwa nyakati tofauti kutokana na Mkutano Mkuu Maalumu kumpitisha Samia kwa kura zote za ndiyo kuwa Mwenyekiti wa CCM na kisha Halmashauri Kuu ya Taifa kupitisha na kuridhia ateue viongozi viongozi mbalimbali.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini ,Dar es Salaam, Dk Lazaro Swai alisema utaratibu wa uchaguzi huo wa juzi jijini Dodoma, umeonesha kuimarika kwa chama na imani kwa Samia.

Kuhusu uteuzi wa viongozi aliofanya, Dk Swai alisema ni jambo la kawaida kwa kiongozi anayeingia madarakani kuchagua timu inayoendana na falsafa yake, imani na maono ya kazi zake na siyo kosa na walioondolewa au kuachwa haimaanishi kuwa hawafai.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda ameipongeza CCM kwa kumchagua Samia kuwa mwenyekiti kwa ushindi wa kishindo.

Shibuda ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Ada-Tadea alisema CCM imeonesha ukomavu, alisema alisema kwa ilani ya chama, ataendeleza fikra za mtangulizi wake, Dk John Magufuli.

Mchungaji wa Kanisa la TAG, Nzuguni Dodoma, Peter Ngh’ombola, alimpongeza Samia na kusisitiza kuwa kilichofanywa na wana CCM kimeonesha kwamba wana imani kubwa naye.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam, Elly Ngailo alisema, uongozi wa juu katika chama unapobadilika wananchi wanatarajia kuona mabadiliko kwa viongozi wa chini hivyo ni kama kuzaliwa upya na hivyo mema mengi yanategemewa.

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi