loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Azam waupania ubingwa wa Simba

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa nia yao kubwa ni kutwaa taji la Kombe la Shirikisho ambalo linashikiliwa na Simba.

Simba pia ndio wanaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na bingwa wa ligi hiyo huliwakilisha taifa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Azam FC inayonolewa na George Lwandamina (pichani)º imetinga hatua ya robo fainali baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Vivien Bahati alisema kuwa bado wanaamini kwamba wana nafasi ya kuendelea kupata matokeo katika mechi zao zijazo.

“Kupita hatua ya robo fainali ni furaha kwetu na bado tuna amini kwamba tuna kazi ya kufanya kwa ajili ya mechi zetu zijazo na tutafanya vizuri.

“Malengo yetu ni kwamba kwenye mechi zetu zilizobaki tutapata matokeo mazuri jambo ambalo litatupa nafasi ya kuweza kulipata taji hili ambalo ni kubwa,” alisema.

YANGA imeendelea kujiweka katika mazingira magumu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi