loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais; Watanzania tumekusikia, tumekuelewa

RAIS Samia Suluhu Hassan juzi alihutubia taifa kwa mara ya kwanza akiwa Rais wa Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyokuwa na kaulimbiu ya kitaifa: “Maslahi Bora, Mishahara Juu, Kazi Iendelee.”

Kitaifa maadhimisho haya yalifanyika jijini Mwanza Rais Samia akiwa mgeni rasmi.

Miongoni mwa mambo aliyoyasema Rais katika maadhimisho hayo na Watanzania kumuelewa kiasi cha kuendelea kumwombea zaidi katika utumishi wake, ni sababu muhimu alizotoa za kutoongeza mishahara mwaka huu ingawa yalikuwa matamanio yake makubwa.

Kwa upendo, unyenyekevu na huruma kwa wafanyakazi na Watanzania kwa jumla, Rais akasema alitamani kutangaza nyongeza ya mishahara, lakini hali imekuwa nje ya uwezo kutokana na changamoto mbalimbali zikiwamo za kiuchumi zilizolikumba taifa hasa hasa, zikisababishwa na ugonjwa wa Covid-19 ulioutikisa ulimwengu kiafya na kiuchumi.

 Sisi tunasema, Watanzania tumemsikia na kumwelewa vizuri rais ndio maana tunamwombea tukiungana naye kukiri ukweli kuwa, ugonjwa huu uliathiri mataifa karibu yote duniani ikiwamo Tanzania na kusababisha athari nyingi hasa.

Ulizifanya nchi kutumia pesa nyingi kupambana na madhara yake kupitia matibabu kwa watu walioathirika na kupata maambuzki ya virusi vya corona na kujenga miundombinu bora katika mifumo ya afya ili  kusambaza vifaa kinga na kutoa sahihi na endelevu kuhusu ya namna ya kuepuka maambukuzi.

Kadhalika, ugonjwa huu kwa Tanzania japo haukuwa na madhara makubwa ukilinganisha na mataifa mengine yanayoteseka hadi sasa, uliathiri uzalishajii mali shambani na katika viwanda kwani muda na idadi ya watu kuingia kazini uliathirika.

Tunasema,  Watanzania tunaungana na ukweli wa rais kuwa hata uingizaji wa bidhaa za kibiashara kutoka nje ya nchi na hata uuzaji wa biadhaa za Tanzania katika soko la nje ya nchi, pia uliathirika kwa kiasi kikubwa kwani nchi nyingi ‘zilifunga milango’ yao ili kuepusha maambukizi zaidi.

Sisi tunasema, kutokana na hali hiyo, uchumi katika nchi nyingi uliyumba na hivyo, kuwa vigumu kufanya nyongeza ya mishahara kwa watumishi na ndio maana tunasema: “Rais Samia; umesema ukweli na Watanzania tumekusikia, tumekuelewa na tunazidi kukuombea maisha bora na utumishi uliotukuka.”

Tunasema Watanzania tunakuuombea ili Mungu akipenda na mambo yakaenda vizuri, matamanio na ahadi yako ya kuongeza viwango vya mishahara mwaka kesho (2022), yatimie ili wafanyakazi waendelee kulitumikia taifa hili kwa moyo wa dhati na kwa ufanisi zaidi.

Ndiyo maana tunapokushukuru na kukupongeza kwa kuwapunguzia mzigo wa kodi ya mashahara wafanyakazi kutoka asilimia tisa hadi asilimia nane, tunasema Watanzania tumeiona nia yako njema, tumekusikia, tumekuelewa na tunakuombea kila la kheri ili ndoto, matamanio na ahadi zako zikitimia.

ZANZIBAR, katika visiwa vyake viwili vya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi