loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

APR, Rayon zaanza ligi kwa ushindi

BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu ya Rwanda, APR na Rayon Sports zimepata ushindi wa kwanza katika ligi hiyo maarufu Primus baada ya kuzifunga Gorilla FC na Gasogi United juzi Jumapili.

APR waliifunga Gorilla FC 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Huye na kuanza vyema mbio zake za kutetea taji hilo.

Kabla ya kuanza kwa mchezo huo, Kocha, Adil Mohamed Erradi na vijana wake walikabidhiwa taji la ubingwa wa msimu wa mwaka 2019/2021 katika sherehe zilizofanyika uwanjani hapo.

Kiungo Keddy Nsanzimfura ndiye aliyeipatia timu hiyo ya jeshi bao la kungoza baada ya dakika 14 ya mchezo kabla mshambuliaji Innocent Nshuti kuongeza uongozi wa mchezo dakika sita baadae.

Jean Claude Nizeyimana alifunga bao la kufutia machozi kwa timu hiyo iliyopanda daraja katika dakika ya 80, lakini walishindwa kulazimisha sare na hadi mchezo huo unamalizika ushindi ulikuwa kwa APR.

Wakati huohuo, mshambuliaji Ernest Sugira aliifungia Rayon Sports bao pekee dhidi ya Gasogi United wakati wa mchezo mkali uliofanyika kwenye Uwanja wa Amahoro.

Gasogi ilikuwa na matumaini ya kugawana pointi hadi pale Sugira alipowatoka mabeki wa Gasogi na kufunga bao hilo la dakika za mwisho ambalo liliiwezesha The Blues kuondoka na pointi zote tatu.

Kesho Jumatano APR watakuwa wageni wa AS Muhanga ambao mchezo wao dhidi ya Bugesera FC uliahirishwa baada ya wachezaji wake karibu 10 kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Rayon kwa upande mwingine itacheza dhidi ya Kiyovu SC ambayo itacheza bila ya kocha wake Oliver Karekezi baada ya mkataba wake kuvunjwa kutokana na kukiuka taratibu za miongozo ya covid-19.

YANGA imeendelea kujiweka katika mazingira magumu ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi