loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri Mkuu kushuhudia pambano la Kiduku, Dulla

SERIKALI imesema itahakikisha inashiriki kwenye pambano la Twaha Kassim ‘Twaha Kiduku’ na Abdalla Pazi ‘Dulla Mbabe’ linalotarajiwa kufanyika Julai, 24, Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi kwenye futari  iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Peaktime Media Entertainment Limited, Seleman Semunyu.

Dk Abbasi akijibu ombi la Semunyu la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi katika pambano hili alisema atalifikisha na anaamini litakubaliwa maana pambano limepangwa kuchezwa tarehe nzuri.

“Serikali tutashiriki kwenye pambano hilo kwa sababu mchezo wa ngumi ni kati ya michezo inayoweza kuitangaza nchi kimataifa. Na kuanzia sasa kama timu inakwenda kuiwakilisha nchi isitarajie kukabidhiwa bendera tu bali itarajie na mengine maana tumetenga bajeti kwa timu za taifa,” alisema Dk Abbasi.

Awali, akimkaribisha Dk Abbasi, Semunyu alisema anashukuru kwa kufanikiwa kuandaa futari hiyo na kuahidi kufanya hivyo kila mwaka na mwakani itakuwa kubwa kuliko mwaka huu.

“Mwanzo nilikuwa nataka kufuturisha watu 50, marafiki zangu wakaniambia hao ni watu waliokuzunguka tu baadae nikasema basi watu 100, nashukuru Mungu niliwashirikisha marafiki zangu na wameniunga mkono hadi kufanikisha,” alisema Semunyu.

Alisema Peaktime imeondoa mchezo wa ngumi Manzese na kuupeleka Masaki na Mlimani City sehemu zenye hadhi na kuwavutia watu wengi zaidi na pambano la kulipa kisasi kati ya Twaha Kiduku na Dulla Mbabe litavuta mashabiki zaidi.

Alisema mara ya mwisho mabondia hao kukutana ilikuwa Agosti 28, mwaka jana, ambapo Kiduku alimpiga Dulla Mbabe hivyo sasa wanataka kuonesha nani zaidi katika pambano la Julai 24.

Naye Shehe wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Musa alisema ni mara yake ya kwanza kufuturu pamoja na mabondia na kusema anashukuru Ramadhan imewaleta pamoja kwa inaonesha upendo, subra na uvumilivu.

YANGA imeendelea kujiweka katika mazingira magumu ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi