loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ziara ya Rais Samia Kenya imalize changamoto zilizopo

Ziara ya Rais Samia Kenya imalize changamoto zilizopo

LEO Rais Samia Hassan Suluhu anaanza ziara ya siku mbili nchini Kenya ikiwa ni safari yake ya pili kutoka ndani ya nchi tangu aliposhika madaraka Machi 19 mwaka huu baada ya kufariki aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Magufuli.

Katika ziara yake ya kwanza, Rais Samia alitembelea Uganda na kukutana na Rais wa nchi hiyo, Yowei Museveni kisha kuweka saini mikataba mitatu yenye nia ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi baina ya nchi hizo mbili.

Serikali za Tanzania na Uganda zilikubaliana katika masuala ya hisa, usafirishaji na ushuru katika hatua za awali za mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta la

Afrika Mashariki la kilometa 1,443 kutoka Magharibi mwa Uganda mpaka kwenye Bandari ya Tanga, Tanzania.

Sasa anaenda nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais Uhuru Kenyatta ambapo watafanya mazungumzo na mwenyeji wake kisha kuhutubia Bunge la nchi hiyo litakalojumuisha wabunge wa mabunge yote mawili ya nchi hiyo.

Rais Samia pia atahutubia Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania utakaofanyika Nairobi kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali yahusuyo fursa za biashara na uwekezaji zilizopo Tanzania na Kenya.

Rais huyo wa kwanza mwanamke katika ukanda wa Afrika Mashariki ameanza kwa kuhakikisha nchi zote za ukanda huo zinakuwa na mahusiano mema na Tanzania ili kuhakikisha changamoto mbalimbali zilizopo zinafanyiwa kazi.

Katika siku za karibuni kumekuwa na changamoto kadhaa baina ya Tanzania na Kenya ziliingia katika

migogoo ya hapa na pale hususan la uingizaji wa mahindi nchini Kenya yakitokea Tanzania kwa madai kuwa na viambata vya sumu.

Kutokana na suala hilo, ililazimika malori kuzuiwa mipakani kwa muda mrefu na kuleta changamoto kwa wasafirishaji na wafanyabiashara wa nchi zote huku Kenya ikielezwa kupata changamoto ya uhaba wa mahindi .

Katika suala hilo ilielezwa kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kuzuia kuingia mahindi kutoka Tanzania na kueleza ilitakiwa hatua zifuatwe mpaka kutangazwa kwa zuio hilo.

Lakini pamoja na mambo mengine kumekuwa na changamoto ndogo ndogo ambazo zinaletia doa uhusiano ya nchi hizo mbili zinazotegemeana kibiashara, huku uchumi wa nchi hizo ukiwa mkubwa na matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa wingi yamesababisha muingiliano wa watu kuwa kwa kiwango kikubwa kuliko 

nchi nyingine za EAC.

Hivyo, kwa ziara hiyo, ni wazi kuwa changamoto zote na jinsi ya kutatua migogoro zitawekwa sawa na watendaji wanaotakiwa kuchukua hatua kuhakikisha wanafanya hivyo mapema kabla ya changamoto zinazojitokeza hazijaathiri watu kwa kiasi kikubwa.

Aidha, kwa wafanyabiashara kukutana na Rais Samia kunaleta mwanga wa kutoa mdukuduku yao katika kukuza biashara za nchi hizo mbili na kisha kwa pamoja serikali zote mbili kufanyia kazi.

Hongera sana Rais Samia kwa kuanza na kuimarisha mahusiano na majirani kisha kuendelea na wadau wengine ili kukuza biashara, utalii na uchumi wa nchi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/75fc51077fff41db539d5cc72dedfe52.jpeg

LIGI Kuu ya Tanzania inaelekea ukingoni ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi