loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Wanaoanza darasa la kwanza wasidaiwe cheti cha chekechea’

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amepiga marufuku kwa shule kudai cheti cha elimu ya awali kwa Wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza.

Alitoa marufuku hiyo bungeni jana wakati wa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Kisangi (CCM), aliyetaka kujua majibu ya serikali kutokana na kuwepo kwa sharti la watoto wanaotaka kuandikishwa darasa la kwanza kutakiwa kuwa na cheti cha kuhitimu elimu ya awali hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Akijibu swali hilo, Waziri Ummy alisema: “Ni marufuku kwa shule kudai ‘certificat’ ya awali kwa wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza. Ninachotaka kusema, bado hatujafanya vizuri kuongeza ‘access’ ya watoto kuanza elimu ya awali, kwa hiyo haileti mantiki kusema kila mtoto anaeanze darasa la kwanza, awe na certificate ya awali,” alisema Waziri.

Akaongeza: “Tunawaahidi wabunge tunaenda kuweka nguvu za kuboresha watoto wetu hususani watoto wa maskini kupata elimu ya awali hususani katika maeneo ya vijijini. Wote wanaodai certificate ya elimu ya awali wajue kwamba wanatenda kinyume na maelekezo na miongozo ya serikali.”

Awali Naibu Waziri wa Tamisemi, David Silinde, alisema serikali inaendelea kuboresha miundombinu na kuwajengea uwezo walimu wanaofundisha elimu ya awali katika shule zote nchini kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.

Silinde aliyesema hayo wakati wa kujibu swali la msingi la Kisangi aliyesema: “Utaratibu wa watoto kuingia darasa la kwanza ni lazima awe amepitia shule za awali.”

Kisangi alitaka kujua mpango wa Serikali kuimarisha madarasa ya elimu ya awali.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi