loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mageuzi sekta ya madini yanavyoboresha barabara

Mageuzi sekta ya madini yanavyoboresha barabara

MOJA ya mambo ambayo Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli atakumbukwa sana ni kuanzisha safari ya mageuzi makubwa katika sekta sekta ya madini.

Kupitia sekta hiyo Watanzania sasa wanaona thamani halisi ya raslimali hizo walizojaaliwa na Mungu katika nchi yao.

Mwaka 2017, Bunge lilifanyia marekebisho Sheria ya Madini ya mwaka 2010 kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 7 ya mwaka 2017.

Hii ilienda sambamba na kuundwa kwa wizara mpya ya madini kwa kuvunjwa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini kupitia Hati ya Majukumu ya Wizara “Instrument” Na. 144 iliyotolewa mwaka 2016 na marekebisho yake kufanyika Oktoba 7, 2017.

Rais Magufuli alihakikisha kunakuwa na marekebisho katika mifumo mbalimbali katika sekta ya madini ikiwemo ya kisheria, kitaasisi na uongezaji thamani ili kuchagiza ufanisi katika kuhakikisha sekta ya madini inalinufaisha taifa.

Kuboreshwa kwa miundombinu muhimu katika maeneo ya migodi ikiwemo ujenzi wa barabara nzuri katika maeneo ya migodi, ujenzi wa ukuta unaozunguka mgodi wa Mirerani, ujenzi wa masoko ya kuuzia madini na mengine ya aina hiyo umesababisha kuongezeka maradufu kwa mapato ya madini.

Lingine la muhimu lililofanyika ni kurekebisha sheria ili kuweka mfumo mpya wa kuwezesha wawekezaji katika sekta ya madini kutoa huduma kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR).

Sasa hivi miji yenye madini kama Kahama, Geita na Tarime unaweza kuona namna mchango wa CSR unavyoinufaisha miji hiyo kutoka na hatua hii kuziongezea uwezo halmashauri mbalimbali nchini mapato.

Mabadiliko ya Sheria ya Madini yameenda sambamba na uboreshaji wa Sheria ya Ushiriki na Uwezeshaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content) na wajibu wa kampuni za uchimbaji madini kuchangia huduma za kiuchumi na kijamii.

Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Charles Marwa, anasema Tarura kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara wanajenga barabara ya lami inayoanzia jirani na mgodi huo mpaka makutano ya Kerende, maarufu kwa jina la Chalinze kupitia CSR.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 2.93 inahusisha ujenzi wa mitaro ya kupitisha maji, makalvati, ufungwaji wa taa za barabarani pamoja na maeneo ya maegesho ya magari katika mji mdogo wa Nyamongo ulio jirani na mgodi huo.

Anasema mpaka kukamilika kwake mradi huo unatarajia kugharimu shilingi bilioni 2.9

Mbali na shughuli za madini kunufaika na barabara hiyo itakapokamilika, watanzaia wanaojihusisha na na ufugaji, uvuvi, kilimo na biashara pia watanufaika kwa kusafirishia mazao na bidhaa zao na hivyo kuchangia katika kunyanyua uchumi wa mkoa.

Uboreshaji wa barabara za mijini na vijijini wilayani Tarime huku kukiwa na mchango wa mgodi wa North Mara umesaidia sana wachimbaji wadogo wadogo, wafugaji, pamoja na wakulima kusafirisha bidhaa zao kutoka sehemu wanapozalishia kwenda kwenye masoko ya uhakika.

Godfrey Kegoye, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi na Fedha wa Halmashauri ya Tarime anaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuleta mageuzi yaliyowezesha mgodi wa North Mara kuchangia kwa kiwango kikibwa maendeleo ya halamshauri kulinganisha na zamani.

Anasema ujenzi wa barabara hiyo unakwenda kubadili taswira ya mji mdogo wa Nyamongo na kwamba usimamizi thabiti utasaidia pia kufanya fedha za CSR zisiliwe na wachache.

Chacha Mwita, mfanyabiashara wa Nyamongo, mji mdogo ulioko Tarime vijijini anasema kujengwa kwa barabara hiyo kutaifanya Nyamongo kuvutia zaidi wawekezaji na kuboresha biashara katika mji huo unaokua kwa kasi.

Mratibu wa Tarura mkoa wa Mara, Mussa Mzimbiri, anasema mwaka 2015, moja ya ahadi za aliyekuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli, ilikuwa ni kuboresha miundombinu, ikiwemo ya mijini na vijijini.

Anasema ahadi ya kujengwa kwa barabara za lami angalau kilomita moja katika halmasahuri za miji na vijiji wameitekeleza katika halmashauri tatu za Rorya, Serengeti pamoja na halmashauri ya Butiama.

“Magufuli alipotoa ahadi ya kuboresha barabara katika halmashauri za mkoa wa Mara, ikiwemo baadhi kwa kiwango cha lami wakati anagombea urais mwaka 2015, ilikuwa kama ndoto lakini wananchi wameshuhudia ukweli na kujionea kwamba takribani katika miji midogo yote barabara nyingi za vumbi zimeboreshwa,” anasema mratibu huyo.

Anasema utekelezwaji wa miradi hiyo uko kwenye bajeti ya shilingi bilioni 1.5 kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020, fedha zilizotolewa na hazina.

Kuanzishwa kwa Tarura anasema ni jambo ambalo limekuwa na manunfaa makubwa katika mkoa wa Mara kwani wameshajenga na kukarabati kadhaa katika kipindi kisichozidi miaka mitatu huku wakifugua njia ambazo awali zilikuwa 

hazipitiki.

Tarura ilichukua majukumu ya kiutendaji kuhusu ujenzi na matengenezo ya mtandao wa barabara za vijijini na mijini yaliyokuwa yakitekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuratibiwa na Idara ya Miundombinu chini ya Tamisemi.

Mratibu Mussa anasema Tarura Mara inashughulikia amtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 4558.98.

Kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020, walikuwa na bajeti ya shilingi 7,527,986,654.19 kwa ajili ya matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 705.90.

Anasema katika mwaka huo wa fedha 2019/2020 Tarura Mara iliidhinishiwa Shilingi 1,309,480,000 kutoka Mfuko wa Barabara kwa kazi za miradi ya maendeleo.

Kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 Tarura Mara ina bajeti ya shilingi 7,771,747,666.21 kwa ajili ya matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 908.99.

Meneja wa Tarura katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Hussen Abbas, anasema mwaka huu wa fedha 2020/2021, moja ya kazi wanayofanya ni kujenga kitako kwa ajili ya kufunga daraja la chuma katika Barabara ya Wanyere – Kataryo unakopita Mto Suguti.

Mradi wa kutengeneza kitako kwa ajili ya kufunga daraja hilo anasema unatarajiwa kugharimu hilingi milioni 74.

Anasema daraja hilo ni muhimu kwa wakazi wa maeneo ya Wanyere na Katearyo kwani wananchi wa upende wa Kataryo hawana huduma za kijamii kama vile vituo vya afya pamoja na shule, hali inayowalazimu kuvuka upande wa pili wa mto ambao ni Wanyere kwa ajili ya kujipatia huduma hizo.

Anasema ujenzi wa daraja hilo unakwenda kuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi hao.

Aidha, Katika Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwa Fedha za Benki ya Dunia, Meneja wa Tarura katika Manispaa ya Musoma, Joseph Mkwizu, anasema, Tarura kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma ilipangiwa shilingi bilioni14.34 kwa ajili ya kujenga barabara ndani ya Manispaa ya Musoma.

Anasema barabara hizo zenye urefu wa kilomita 11.381 zimejengwa kwa lami nzito na kuwekewa taa zinazotumia sola zipatazo 328.

“Pia tumejenga vibanda 12 vya kupumzikia watumiaji wa barabara,” anasema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/bb8c33e5fefda6a32b573830ba0d94ae.png

WAFUGAJI wa ng'ombe wa maziwa nchini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi