loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Eneo la umwagiliaji nchini laongezeka- Serikali

Eneo la kilimo cha umwagiliaji limeongezeka na kufikia hekta 695,045 katika kipindi cha mwaka 2019/20 na 2020/21, Serikali imebainisha.

Hatua hiyo imechangia kufikia asilimia 58 ya lengo la kufikia hekta milioni 1.2 ifikapo 2025.

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliyasema hayo jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Agnesta Kaiza.

Katika swali lake, Mbunge huyo alihoji serikali ina mkakati gani wa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji katika mikoa ya Kigoma, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma na Morogoro ili kuongeza mazao ya kilimo yatakayosafirishwa kupitia Reli ya kisasa ya mwendokasi(SGR).

Akijibu swali hilo, Bashe alisema ongezeko hilo limetokana na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu ya Kilangali Seed Farm (Kilosa) kupitia mradi wa ERPP na skimu 13 za SSIDP kupitia mradi wa SSIDP.

Amesema Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea kutekeleza kilimo cha umwagiliaji katika mikoa inayopitiwa na SGR kuanzia Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanza, Tabora na Kigoma ili kutathmini maeneo yote ya uzalishaji na kuhakikisha kuwa miundombinu sahihi inajengwa katika maeneo hayo.

"Ili SGR itakapokamilika iweze kutumika katika kusafirisha mazao ya kilimo. Serikali imekamilisha ujenzi wa awali kwa skimu za umwagiliaji ya Nyida (Shinyanga), Mwalunili (Igunga), Gwanumpu (Kakonko), Itagata (Singida), Mvumi na Kilangali (Kilosa), Dakawa na Kigugu (Mvomero) na Msolwa ujamaa na Njage (Kilombero),"alisema.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi