loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zanzibar yaendelea kupitia uwiano wa sera elimu kimuungano

WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia imesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafanya mapitio ya Sera ya Elimu ili kuweka uwiano wa miaka kwa elimu ya msingi baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Omar Kipanga alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum (CCM), Najma Murtaza Giga.

Katika swali, Giga alihoji Kama serikali haioni umuhimu wa kuwa na Sera na Mitaala shirikishi ili kuwa na msingi wa aina moja kuanzia elimu ya maandalizi, elimu msingi na sekondari kati ya Tanzania Bara na Zanzibar ili kuongeza ufaulu zaidi kwa upande wa Zanzibar.

Akijibu swali hilo, Kipanga alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikishirikiana vizuri na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo suala la elimu hususan katika utekelezaji wa mitaala na kutoa elimu bora kwa watoto wa Kitanzania.

"Kuhusu sera na mitaala shirikishi baina ya pande mbili za Muungano, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) hushirikiana na Taasisi ya Elimu Zanzibar (TEZ) katika masuala mbalimbali yahusuyo utekelezaji wa mitaala,” amesema.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi