loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yaitaka Bodi ya mikopo kuondoa adhabu ya 10% kwa wanaochelewesha mikopo

SERIKALI imeiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuondoa tozo ya adhabu ya asilimia 10 ya mkopo ambayo inatozwa kwa wanufaika wanaochelewa kulipa mikopo kwa wale walionufaika.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa Joyce Ndalichako wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Waziri huyo ametoa agizo hilo ikiwa ni siku chache baada ya Rais Samia Suluhu kufuta tozo ya asilimia sita ya mikopo iliyokuwa ikitolewa na bodi hiyo.

Katika utekelezaji wa agizo hilo, Profesa Ndalichako amesema Serikali itaondoa tozo ya asilimia sita ya kulinda thamani ya fedha katika urejeshaji wa mkopo, itaondolewa kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Amesema Serikali inaiagiza Bodi ya Wakurugenzi  kuondoa pia tozo ya adhabu ya asilimia 10 ya mkopo ambayo inatozwa kwa wanufaika wanaochelewa kulipa mikopo hiyo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi