loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mitaala elimu kuanza kutathminiwa ili kuendana na wakati

SERIKALI ipo mbioni kufanya ufuatiliaji na tathmini ya kina ya mitaala inayotumika kwa sasa ili kuhakikisha kuwa ufundishaji na ujifunzaji unafanyika kwa kuzingatia viwango na vigezo vilivyowekwa.

Ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa Joyce Ndalichako wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Waziri Ndalichako amesema kuwa vigezo hivyo ni pamoja na uwepo wa walimu kulingana na idadi ya wanafunzi, vitabu na mazingira ya kujifunzia.

Pia amesema Serikali itaanza kufanya mapitio ya mitaala katika ngazi zote za elimu ili kuhakikisha kuwa elimu na mafunzo yanayotolewa yanajikita katika kujenga ujuzi na kuzingatia mahitaji ya sasa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi