loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ummy: Nitakula na nyie sahani moja, hakuna atakayechomoka

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamiesemi) Ummy Mwalimu,  amesema atakula sahani moja na mtumishi atakayeharibu na kuhama kituo chake cha kazi.

Amesema baadhi ya watumishi wa Tamisemi hawana weledi na wamekuwa wakifanya ubadhilifu katika miradi kisha wanaomba kuhama vituo vya kazi ili kukwepa kujibu tuhuma.

“Tamisemi walizoea kufanya ubadhirifu wa miradi ya maendeleo haswa ya Elimu, Afya na Barabara na wakishaona mradi haujakamilika au unatuhuma hizi na zile anahama,  sio wakati wa uongozi wangu hakuna atakayehama kukwepa tuhuma.” alisema Ummy na kuongeza

“Na hapa Chemba wote waliohama sababu ya kutokukamilisha miradi ya maendeleo kama Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya watarudi  kuja kujibu tuhuma zao” alisisitiza

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Mei 4, 2021 katika ziara yake wilayani Chemba mkoani Dodoma kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na Kamati ya Fedha  pamoja na Menejimenti ya Halmashauri  hiyo leo Mei 5, 2021.

Akisisitiza Waziri Ummy alisema  “Sitaruhusu  mtumishi aharibu Chemba kisha ahamishiwe Kongwa, niwahakikishie kuwa nitamshughulikia akiwa hapa hapa Chemba na nikibaini ana hatia nitamchukulia hatua stahiki”.

Ummy yupo katika ziara hiyo  kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na kamati za Fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Bahi na kongwa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi