loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vipaumbele 10 vya bajeti ya Elimu hivi hapa

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako ametaja vipaumbele 10 vya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022

Akiwasilisha bajeti yake Bungeni leo, Waziri Ndalichako aliomba Bunge limuidhinishie Shilingi trilioni 1.38 ili iweze kutekeleza vipaumbele vyake katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Alitaja vipaumbele  ambavyo watavifanyia kazi katika mwaka wa fedha 2021/2022 kuwa ni kufanya mapitio  ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 kwa lengo la kuhakikisha kuwa inakidhi mahitaji ya sasa.

Alisema pia  Serikali itafanya mapitio ya Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 ili kuhakikisha inaendana na mazingira ya sasa ya utoaji wa elimu nchini.

“Pia, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali itaweka msisitizo zaidi katika ufundishaji wa masomo ya ufundi kwa kuimarisha mafunzo kwa vitendo katika shule za sekondari za ufundi.” alisema

Amezitaja shule hizo ni  Iyunga, Ifunda, Tanga, Bwiru Wavulana, Musoma, Mwadui, Moshi na Mtwara.

“Vilevile, Serikali itaimarisha ufundishaji wa masomo yanayowajengea wanafunzi ujuzi katika shule za msingi na sekondari.”

“Masomo hayo ni pamoja na Kilimo, ufundi, stadi za kazi, michezo, na biashara,” alisema Profesa Ndalichako.

Aidha kipaumbele kingine alichokitaja ni kutilia mkazo ufuatiliaji na tathmini ya kina ya mitaala inayotumika kwa sasa ili kuhakikisha ufundishaji na ujifunzaji unafanyika kwa kuzingatia viwango na vigezo vilivyowekwa.

“Vigezo hivyo ni pamoja na uwepo wa walimu kulingana na idadi ya wanafunzi, vitabu na mazingira ya kujifunzia.

“Serikali itaanza kufanya mapitio ya mitaala katika ngazi zote za elimu ili kuhakikisha kuwa elimu na mafunzo yanayotolewa yanajikita katika kujenga ujuzi na kuzingatia mahitaji ya sasa,” alisisitiza.

Waziri huyo amesema, mwaka 2021/22, Serikali itafanyia kazi maoni na ushauri wa wadau wa elimu kuhusu utekelezaji wa sheria ya mwaka 2018 iliyounda bodi ya kitaalamu ya walimu.

“Aidha, Serikali itazingatia pia maoni na ushauri wa kamati ya kudumu ya bunge ya sheria ndogo walioutoa katika majadiliano kuhusu kanuni za bodi ya kitaalamu ya walimu yaliyofanyika tarehe 28 Aprili 2021 kati ya Wizara ya Elimu na Kamati hiyo,” amesema Profesa Ndalichako.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi