loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

HakiElimu watoa mapendekezo 5 kuboresha elimu nchini

SAA chache baada ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuwasilisha bajeti ya Sh trilioni 1.38 kwa mwaka wa fedha 2021, Shirika la HakiElimu  nchini limetoa mapendekezo yake matano.

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dk John Kalage ameyataja mapendekezo hayo kuwa ni pamoja na Kuongeza Bajeti kuwasaidia watoto wa kike kutatua changamoto zinazowakabili  ikiwemo kuwasaidia kupata mahitjai yao zikiwepo taulo za kike.

Mapendekezo mengini ni kuongeza bajeti ya miundombinu kwa kuzingatia vipaumbele vya madarasa na mahitaji ya shule, Kuweka nguvu na bajeti kwenye suala la uthibiti ubora, Kusimamia sula la upungufu wa walimu kwa kuajiri walimu wapya na kuzingatia mgawanyo sawa wa walimu, vilevile kulitazama suala la kikokotoo cha ruzuku.

Alisema pendekezo lingine la HakiElimu ni kupandisha ruzuku kutoka Sh 10,000 mpaka  Sh 25,000 kwa shule za Msingi na kutoka  Sh 25,000 ya sasa mpaka Sh 50,000 kwa shule za sekondari.

Aidha alisema, “Tunatambua kuwa, Bajeti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya Mwaka 2021/2022 iliyopitishwa imebainisha kukamilisha maboma ya madarasa 3,268 ili kukabiliana na changamoto ya miundombinu kwenye shule za msingi ambayo ni sawa na asilimia nne tu ya upungufu wa madarasa 82,200.

“Ili kutatua uhaba wa madarasa kwenye shule za msingi inahitaji uwezekaji mkubwa sana wa takribani shilingi  trilioni 1.6, na njia pekee ni kuwa na mpango maalumu wa miaka minne kati ya 2021/2022 hadi 2024/2025 kupanga bajeti ya shilingi bilioni 400 kila Mwaka wa Fedha kujenga madarasa 20,000 kila mwaka ili kuondoa uhaba wa madarasa ifikapo Mwaka 2025," alisema

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi