loader
Dstv Habarileo  Mobile
CAF yaruhusu wachezaji 9 wa akiba

CAF yaruhusu wachezaji 9 wa akiba

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeongeza idadi ya wachezaji wa akiba kutoka saba hadi tisa kuanzia hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika inayotarajiwa kuanza kuchezwa Mei 14, mwaka huu.

Kuhusu idadi ya wachezaji watakaoruhusiwa kuingia kwenye mechi moja, CAF imesema klabu zitataarifiwa baada ya marekebisho yanayotarajiwa kufanywa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kupitia IFAB (Bodi ya Vyama vya Soka vya Kimataifa) ambao wanahusika na marekebisho ya sheria za soka na kanuni.

Mashirikisho ya soka ya kila nchi yametaarifiwa kuziambia klabu zitakazoshiriki mashindano yajayo ya msimu wa mwaka 2021/2022 kuthibitisha ushiriki wao kwa Kamati ya Mashindano ya CAF kupitia CMS (mfumo wa usimamizi wa mashindano) sio zaidi ya Juni 30, 2021.

Taarifa hiyo ilisema usajili wa wachezaji mwisho itakuwa ni Julai 10 bila faini na kipindi cha pili ni itakuwa kati ya Julai 11-20 kwa faini ya dola za Marekani 250 kwa mchezaji mmoja.

Aidha, kipindi cha tatu cha usajili itakuwa ni kuanzia Julai 21-31, ambapo vyama havitaruhusiwi kuondoa jina la mchezaji yeyote bali kuongeza mapya, huku faini ikiwa ni dola za Marekani 500 kwa mchezaji mmoja na utaratibu huo utaanza kutumika katika hatua ya pili ya raundi za mwanzo na kuendelea.

Kuhusu leseni za makocha, CAF imesema kocha mkuu lazima awe na leseni A ya CAF au Pro-License na kocha msaidizi lazima awe na leseni B ya CAF na kuendelea kwa mashindano yote ya shirikisho hilo

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/12f1ecfe03051e3f01f4f959e93b9181.jpg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi