loader
Dstv Habarileo  Mobile
Baba wa kambo amchoma  kisu mtoto, ajinyonga

Baba wa kambo amchoma kisu mtoto, ajinyonga

MKAZI wa mtaa wa Nyantorotoro, kata ya Nyankumbu wilayani Geita Shija Mwanzalima (30) anadaiwa kumchoma kisu mwanawe wa kambo na yeye kujiua kwa kujinyonga.

Tukio hilo limethibitishwa na Polisi Mkoa wa Geita . Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, mtoto aliyechomwa kisu ni Rechel Erasto mwenye umri wa miaka mitatu na miezi mitano.

Kamanda Mwaibambe alisema mtoto huyo alipata jeraha kubwa tumboni na alilazwa Hospitali ya mkoa wa Geita na hadi sasa hali yake inaendelea vizuri baada ya kushonwa.

Kamanda huyo alisema baada ya mwanaume huyo kumchoma kisu mwanawe wa kambo alijijichoma kisu tumboni na baadaye akaingia chumbani akajinyonga na akafariki dunia.

“Mbinu aliyotumia huyu marehemu, alimtuma mke wake, kwamba aende dukani kumnunulia mtoto dawa, kwa hiyo mke alipoenda dukani, huku nyuma yake ndio kukatekelezwa tukio hilo, mume akamjeruhi mtoto na yeye akajinyonga.

“Chanzo cha tukio hili ni msongo wa mawazo, huyu marehemu na huyu mwanamke wameoana hivi karibuni, huyo mtoto siyo wa kwake, baada ya kuoana walienda kupima afya hospitalini, na ikabainika mwanaume ana maradhi na mke yupo salama, na huyu mwanamme alikuwa anaishi kwa mwanamke,”alisema Kamanda Mwaibambe.

Ofisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Mji wa Geita, Carthbert Byabato alikiri uwepo wa ongezeko la vitendo vya ukatili. Alisema changamoto hiyo inatokana na ongezeko la msongo wa mawazo miongoni mwa watu hivyo aliishauri jamii kujitahidi kuishi kwa amani na utulivu kuepuka matukio hayo

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/fd2b4b01dfd5c4a2ec112299883be99f.jpg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ...

foto
Mwandishi: Yohana Shida, Geit

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi