loader
Dstv Habarileo  Mobile
Uongozi Coastal wamkingia kifua Juma Mgunda

Uongozi Coastal wamkingia kifua Juma Mgunda

UONGOZI wa Coastal Union umewaomba mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuendelea kumpa ushirikiano kocha wao, Juma Mgunda (pichani) kwani bado yupo klabuni hapo.

Kauli hiyo ya viongozi wa Coastal imekuja siku chache baada ya kuzagaa kwa tetesi kwamba klabu hiyo imeachana na kocha huyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo yenye makao yake mkoani Tanga, uongozi umesikitishwa na taarifa za uzushi za kufukuzwa kwa kocha huyo ambaye kwa kipindi kirefu amekua akifundisha kikosi hicho.

“Uongozi wa Coastal Union unakanusha taarifa iliyozua taharuki kubwa kwa mashabiki kuhusu kufukuzwa kwa kocha mkuu, Juma Mgunda ambayo ilisambazwa kupitia 

kipeperushi chenye maneno ya Kiingereza ‘Breaking News, Juma Mgunda out’ kitu ambacho hakina ukweli wowote,” ilisema taarifa hiyo.

Uongozi wa timu hiyo umewataka wanachama na mashabiki kupuuza uzushi huo uliotungwa na watu wachache wasioitakiwa mema klabu hiyo.

Pia uongozi huo umelaani kitendo hicho ulichosema si cha kiungwana na kwamba Mgunda ataendelea kuinoa Coastal Union hivyo mashabiki wanaombwa kuendelea kumuunga mkono pamoja na wachezaji ili waweze kufanya vizuri katika michezo ya Ligi Kuu iliyobaki.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d5ccf730753a628a62cbcb16e94f9163.png

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi