loader
Dstv Habarileo  Mobile
Muungano lulu yetu; tuutunze, tuulinde kwa nguvu zetu zote

Muungano lulu yetu; tuutunze, tuulinde kwa nguvu zetu zote

TAREHE 26 mwezi wa April, 1964 haitasahaulika mioyoni mwa Watanzania kwa kuwa ni siku ambayo nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizaliwa baada ya kuunganisha mataifa mawili ya Tanganyika na Zanzibar.

Kazi kubwa iliyofanywa na wazee wetu Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Karume ilitosha kabisa kutuunganisha watanzania.

Tangu kuzaliwa kwa taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miaka 57. Umri huu ni mkubwa sana na laiti kama angekuwa ni mwanadamu tungesema ni mtu mzima anayeelekea kwenye uzee.

Hali hii inafanya zaidi ya asilimia 60 ya watanzania wote kuwa ‘Watanzani’, yaani walizaliwa ndani ya Muungano. Kwa kugha nyingine kea sasa tuna watanzania wachache waliozaliwa kabla ya muungano.

Faida za muungano wetu ni nyingi sana kwa pande zote mbili kuanzia siasa hadi uchumi na tamaduni. Hivyo ipo kila haja ya kuulinda muungano huu.

Natambua kuna nyakati baadhi ya wanasiasa wetu uchwara waliongea mambo mabaya kuhusu muungano huu, waliubeza na kujaribu kuwachonganisha watanzania na viongozi wao kuvunja muungano wetu.

Watu hawa ni wa kukemea kama tukemeavyo mapepo kwa kila namna na kuwakumbusha kwamba hakuna Tanzania bila Muungano. Kama Hayati Baba wa Taifa alivyowahi kusema, nje ya Muungano kuna makabila madogo madogo na siyo nchi. Nchi yetu ilipofikia sasa haipaswi kurejea nyuma na kuhatarisha muungano wetu.

Ni wazi kwamba lile kundi la G55 bado linatamani ndoto yao waliotaka itokee mwaka 1993 ifanikiwe sasa au siku zijazo; lakini kama walishindwa wakati ule watashindaje sasa? Kundi hili au wenye mawazo kama waliyokuwa nayo watu wa kundi hili ni wa kudhibitiwa kwa kila namna.

Baada ya kifo cha Rais Magufuli walianza kuleta hoja yao tena kwa mara nyingine inayoleta chokochoko katika Muungano wetu lakini Mungu ni mwema kwamba Rais Samia ameweza kuizima ajenda hiyo kwa sasa.

Maneno aliyoyatumia Rais Samia kuwakemea yalifanana na haya:

Ole wake Tanzania, Tusipoisaidia! Niwezalo nimefanya: Kushauri na kuonya. Nimeonya: Tahadhari! Nimetoa ushauri: Nimeshatoka kitini; zaidi nifanye nini.

Namlilia Jalia, Atumulikie njia; Tanzania ailinde, Waovu wasiivunde.

Nasi tumsaidie, Yote tusiyamwachie! Amina, tena Amina! Amina tena na tena! maneno haya yanapatikana kwenye kitabu cha uongozi wetu na hatma ya Tanzania kilichoandikwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Nimependa kuyatumia maneno haya ya Mwalimu Nyerere kutokana na uzito wake na maana kubwa ambayo maneno hayo yanaibeba. Kimsingi mbali ya kwamba mzee huyu amekwishatangulia mbele ya haki lakini maneno yake na misimamo yake pamoja na hoja zake alizozitoa wakati wa uhai wake vinamfanya azidi kuishi katika Tanzania yetu na ulimwengu wote kwa ujumla.

Wakati wa Uhai wake, hakuuonea aibu muungano wetu hata siku moja na hadi anaingia kaburini alikuwa anaupigania kwa nguvu zake zote, hasa tukirejea kile kilichotokea mwaka 1993 wakati wa G55!

Na wakati Zanzibar imejiunga na OIC! Mzee huyu alihakikisha kwamba wenzetu wanarudi na kutokubali kuuvunja undugu wetu ambao tumekuwa nao kwa muda mrefu hata kabla ya kuja kwa mabeberu katika nchi yetu.

Nafurahishwa kwamba jitihada za wafuasi wake zimeendelea kuzingatia yale aliyoaamini Mzee wetu Nyerere na mwenzie, Karume.

Wakati wa maadhimisho ya miaka 53 ya muungano wetu Rais Magufuli alisema:

Muungano ndiyo silaha yetu; Muungano ndyo jembe letu; muungano ndiyo umoja wetu, Muungano ndiyo ushindi wetu. Nataka niwahakikishie mimi pamoja na Dk Shein tutaulinda muungano kwa nguvu zote na kamwe asijitokeze mtu yoyote atakayejitahidi au kujaribu kuuvunja muungano, atavunjika yeye.

Maneno haya aliyasema wakati akihutubia siku ya Muungano wetu. Pamoja na vuta ni kuvute za kisiasa Magufuli alihakikisha analinda muungano wetu na kuudumisha kama moja ya tunu zetu watanzania.

Wakati wa kuapisha mawaziri mwezi Machi, Rais Samia aliseleza haya: “Wizara ya Mambo ya Nje mnafanya kazi kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na mnajua kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ya pande zote mbili. Naombeni mind (fikra) zikae hivyo, kwamba mpo kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na hili nalisema kwa mawaziri na makatibu wakuu wote.

Tangu kuapishwa kwake Rais Samia ameonyesha jitihada za wazi kulinda na kudumisha muungano wetu. Kinachohitajika sasa ni kuzidi kumuunga mkono na kumwombea kwa Mwenyezi Mungu azidi kumuongoza kwa hekima kubwa ili azidi kuulinda muungano wetu.

Kuna nadharia potofu ambayo imekuwa ikihubiriwa na baadhi ya wanasiasa uchwara ya kutaka kuhusanisha Muungano wetu na Chama Cha Mapinduzi kwamba huu ni muungano wa chama hiki tawala na siyo wa watanzania. Dhana hii ni potofu na inapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Japokuwa ni ngumu kutenganisha historia ya nchi yetu na chama tawala lakini haimaanishi kwamba huu ni muungano wa chama bali ni muungano wa watanzania wote. Wanasiasa wa namna hii wanakuwa na lengo moja tu la kutaka kuwagawa watanzania kwa sababu ya itikadi za kivyama. Ili watumie fursa hiyo kushinda kwenye chaguzi

furaha yangu ni kwamba pamoja na mambo mengine CCM imejitahidi uhakikisha inalinda heshima ya wapigania uhuru wa nchi hii na wana mapinduzi katika kipindi chote hiki. Kazi hii inapaswa kuendelezwa.

Sasa kilichobaki ni kusambaza elimu ya historia ya nchi yetu ili kuwafanya vijana ambao ni asilimia kubwa ya watanzania kuifahamu nchi yao vyema na kuheshimu na kulinda muungano wetu bila kuuonea aibu kwa namna yoyote ile.

Kuhoji muungano wetu kwa kizazi cha baada ya muungano huo ni sawa na mtoto kumhoji mzazi wake hali ilikuaje kabla ya kutungwa mimba yake. Huu ni utovu wa nidhamu.

Kama watanzania tutumie muungano wetu adhimu duniani kujiimarisha na kujitangaza kama taifa lenye nguvu ya umoja isiyoteteleka kupitia muungano huo.

Mwandishi wa makala haya ni mchangiaji wa gazeti hili. Mawasiliano +255-71224-6001 flugeiyamu@gmail.com

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5d13c5ed3c6fa6cd210b18ef22fa61d9.jpeg

WAFUGAJI wa ng'ombe wa maziwa nchini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ...

foto
Mwandishi: Felix Lugeiyamu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi