loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tozo za umeme Zanzibar kutafutiwa ufumbuzi

Tozo za umeme Zanzibar kutafutiwa ufumbuzi

TIMU za wataalam wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kwa pameja wameshawasilisha katika Kamati ya Wizara zinazoshughulikia masuala ya Muungano ili kufanyia kazi mapendekezo ya tozo za umeme kwa wananchi wa Zanzibar.

Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato wakati akijibu swali la Mbunge wa Jang’ombe aliyehoji ni lini Serikali itatatua mgogoro wa bei ya umeme unaotumika na Watanzania waishio Zanzibar ili kuweka usawa kwa Watanzania wote. 

Byabato amesema kuwa  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeendelea kushughulikia suala la bei ya kuuza na kununua umeme baina ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) ili kuupatia ufumbuzi changamoto hiyo. 
Amesema, “Katika kipindi cha mwaka 2020/21 timu ya wataalamu wa taasisi husika zilikutana katika vikao mbalimbali na kufanya uchambuzi wa kina wa vigezo vilivyohusika katika kupanga bei hiyo ya kuuzia umeme kwa wateja wakubwa wa kununua umeme ikiwemo ZECO. 

“Kutokana na uchambuzi huo, inapendekezwa kuwa vigezo hivyo vipitiwe upya ili kuleta unafuu kwa wateja wa aina hiyo ikiwemo ZECO,” amesema Naibu Waziri huyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5e2df8d01121622c996db31e2bbad601.jpg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi