loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wavuvi watakiwa kupaza sauti kupitia vyama vya ushirika

Wavuvi watakiwa kupaza sauti kupitia vyama vya ushirika

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imewataka wavuvi kujiunga kwenye vyama vya ushirika ili waweze kupaza sauti ya pamoja ili kufikiwa kirahisi lakini pia kutatua changamoto zinazowakabili pamoja na kuwa na usimamizi endelevu wa rasilimali za uvuvi.

Hayo yamebainishwa bungeni leo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati akijibu swali la Mbunge wa Nyasa, Stella Manyanya alitaka kujua ni kwa nini mikopo ya injini za boti isitolewe kwa mtu mmoja mmoja aliye tayari badala ya kutoa kupitia vikundi.

Akijibu swali hilo, Ulega amesema ibara ya 43 (h) ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 inaelekeza serikali kuhamasisha uanzishaji na uimarishaji wa vikundi na vyama vya ushirika vya msingi vya wavuvi wadogo kwa lengo la kuwapatia mtaji, ujuzi, vifaa pamoja na zana za uvuvi.

"Serikali imekuwa ikiviwezesha vyama vya ushirika kwa kuvipatia elimu, zana na vifaa bora za uvuvi hususan injini za boti pamoja na kuviunganisha na taasisi za kifedha ili kupata mikopo yenye riba na masharti nafuu kwa lengo la kufanya shughuli zao kwa tija,"amesema Ulega.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/8d9b98e4478af8bf0de86a883a3e3aab.jpg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi