loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mavunde awakumbuka dereva Taksi

Mavunde awakumbuka dereva Taksi

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde leo amekabidhi sare kwa kituo cha madereva taksi wa Uwanja wa Ndege Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma ya usafirishaji jijini humo.

Mavunde amekabidhi sare kwa madereva taksi 30 zenye thamani ya Shilingi milioni 1.5 katika eneo la Uwanja wa Ndege kwa lengo la kuwafanya madereva hao kuwa nadhifu na kutambulika kwa urahisi kwa wageni waingiao Dodoma kupitia Kiwanja hicho cha Ndege.

“Kwa kuwa ninyi mnapokea wageni kutoka maeneo mengi tofauti nchini na duniani,  ni vyema mkawa na utambulisho mzuri kupitia sare na pia kuwa nadhifu muda wote ili wageni waingiapo wapate sura halisi ya Dodoma kupitia ninyi.” alisema na kuongeza

“Kwa kuwa Dodoma sasa ni makao makuu ya nchi, yatupasa kuboresha huduma hizi za usafiri kwa kuonyesha utofauti na maeneo mengine kwa kuanzia kwenye unadhifu wa mavazi mpaka ukarimu kwa wageni wetu.” alisisitiza Mavunde

Aidha, alisema yupo mbioni kuratibu semina kwa ajili ya mafunzo ya ukarimu kwa watoa huduma mbalimbali katika jiji hilo ikiwemo sekta ya usafirishaji.

Alisema lengo ni kuona huduma mbalimbali zinaenda na kasi ya ukuaji wa jiji na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Taksi-Uwanja wa Ndege Dodoma,  Lotson Mushobozi Nkongo amemshukuru Mbunge huyo kwa kuwajali watoa huduma ya usafiri katika kituo hicho cha Uwanja wa Ndege, kutoa huduma bora kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kulinda sifa ya Makao makuu ya nchi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/0347328c0435aa43d585989b2cf07bfe.jpg

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi