loader
Dstv Habarileo  Mobile
MAJALIWA AWAPA NENO WAPIGA KURA BUHIGWE, MUHAMBWE

MAJALIWA AWAPA NENO WAPIGA KURA BUHIGWE, MUHAMBWE

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameomba wanachi wa Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma wamchague mgombea ubunge kwa tiketi cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Felix Kavejulu katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 16 mwezi huu.

Waziri Mkuu alisema hayo jana katika uwanja wa shule ya msingi Buhigwe kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya kuwania ubunge wa jimbo la Buhigwe.

Jimbo hilo lipo wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa hapo Dk Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais.

“Wana-Buhigwe wote bila ya kujali vyama vyenu nawaomba kura zenu. Tarehe 16 itakapofika mumpigie kura mgombea wa CCM, kwani mnapomchagua mwakilishi si wakati wa kuleta mzahazaha lazima tumchague mtu atakayekuwa tayari kututumikia”alisema Majaliwa. Naye mgombea Kavejulu alisema anazifahamu kero zote za wakazi wa jimbo hilo na kuwataka wampee fursa ya kuwawakilisha bungeni.

“Naomba mnitume kazi, yani nina uwezo wa kuwafanyia kazi yena kubwa na kwa ufanisi kinachotakiwa ni kuniamini na kunichagua ili niwavushe, hakika ninazijua kero na zinanikera sasa ni muda wa kuzimaliza, naomba mnichague”alisema Kavejulu.

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi