loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tambo kibao Simba, Yanga

Tambo kibao Simba, Yanga

TAMBO zimeendelea kwa wachezaji, mashabiki, viongozi na wapenzi wa soka wakati huu wa kuelekea mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Tambo hizo zimezima kwa muda vita ya kushuka daraja ambayo imeendelea kuwa ngumu kwa JKT Tanzania, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, ambazo huenda msimu ujao wa 2021/2022 zisiwapo katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Huu ni msimu wa 57 tangu Ligi Kuu ya Tanzania Bara ilipoanza rasmi kama mashindano mwaka 1965, ambapo hadi sasa timu hizo zimekutana mara 107, huku Yanga ikiibuka na ushindi mara 37, Simba ikishinda mara 32 na sare mara 38.

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gwambina mjini Misungwi hivi karibuni, mabingwa watetezi Simba wamefikisha pointi 61 wakiwa na michezo tisa mkononi, ikiwa imecheza michezo 25, huku Yanga itashuka uwanjani katika mchezo huo ikiwa nafasi ya pili na pointi 57 kibindoni baada ya mechi 27, ikibakiwa na mechi saba.

Simba ikishinda mechi zote tisa ilizobakinazo mkononi ikiwamo dhidi ya Yanga, itakuwa imejikusanyia pointi 27, hivyo zikichanganywa na ilizonazosasa yaani 61 itamaliza msimu na jumla ya pointi 88 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

Simba imeshinda mechi 16 katika michezo 22 iliyocheza, ikipata sare nne nakupoteza mara mbili, ikiwa na maana imedondosha pointi 14 tu, ikiwa na michezo mitatu mkononi kuifikia Yanga iliyocheza 25 na kukusanya alama 54.

Na endapo Yanga itashinda mtanange huo itakuwa imefikisha pointi 60 ikiwa ni pointi moja nyuma ya Simba hivyo kuongeza presha ya kurudi kileleni endapo Wekundu hao wa Msimbazi watatereka kidogo mechi zake zijazo na wao kuendeleza ushindi.

Yanga imebakiwa na michezo saba baada ya juzi kuipiga 1-0 Biashara United. Katika mechi zake 27 za awali, Yanga imeshinda 16 kutoka sare 9 na kupoteza mchezo mmoja pekee, huku ikibakiwa na michezo saba.

Iwapo itashinda mechi zote itakusanya pointi 21, ukichanganya na 57 ilizonazo sasa, itakuwa imefikisha pointi 78.

Nyota wa klabu hizo mbili wameendelea kutambiana huku kila mmoja akiapa kuipigania timu yake ili kuondoka na pointi tatu na kuongeza mbio za kulisaka taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Saido Ntibazonkiza amesema huu ndio wakati wao wa kupunguza idadi ya pointi baina yao na kuongeza presha ya kulisaka taji la Ligi Kuu ambalo linashikiliwa na watani wao hai wa jadi.

Naye mlinzi kisiki wa timu hiyo, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amesema mchezo huo ni kipimo sahihi kwake kuonesha ubora wake kwa kuisaidia timu yake kuondoka na pointi tatu ili kurejesha morali ya upambanaji kikosini na kutwaa taji la Ligi Kuu.

Mshambuliaji na nahodha wa Simba, John Bocco amesema kila kitu kinaenda vyema kambini kwao, wachezaji wana morali ya upambanaji na watautumia mchezo huo kulipa kisasi baada ya kupoteza kwa penalti 4-3 katika michuano ya Kombe la Mapinduzi na kupoteza taji hilo.

Naye mlinda mlango wa timu hiyo, Aishi Manula alisema huu ni wakati wa kuonesha ukubwa wa Simba kwa kushinda kila mchezo ulio mbele yao kwa kuendeleza wimbi la ushindi kama walivyofanya katika michezo mitano iliyopita.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/bfa814f3c58917df1e509befe27f0f89.jpeg

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi