loader
Dstv Habarileo  Mobile
MTANZANIA KUZICHEZESHA PIRATES, RAJA

MTANZANIA KUZICHEZESHA PIRATES, RAJA

MWAMUZI msaidizi wa Tanzania mwenye beji ya Fifa, Frank Komba ni miongoni mwa waamuzi watakaochezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Orlando Pirates dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco.

Mchezo huo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa Mei 16, Orlando Pirates watakuwa nyumbani katika Uwanja wa Ellis Park, Gauteng jijini Johannesburg.

Huu ni mwendelezo mzuri kwa Komba ambaye pia alikuwa miongoni mwa waamuzi waliochezesha fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, (Afcon U20) mwaka huu nchini Mauritania.

Komba ameendelea kuwa mfano kwa waamuzi wengi wa kitanzania kutokana na uimara wake na kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika michuano mbalimbali mikubwa Afrika.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fdc9fb414c28c8c4a258fd0fad8913d8.jpeg

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi