loader
Dstv Habarileo  Mobile
JKT YASHINDA NYUMBANI

JKT YASHINDA NYUMBANI

TIMU ya JKT Tanzania imetumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri, Dodoma baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC kutoka Ilulu mkoani Lindi.

Mchezo huo wa kiporo umekuwa mchezo wa tatu kuzikutanisha timu hizo katika michuano miwili tofauti ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Azam, ambapo Namungo imefanikiwa kushinda mara mbili na JKT Tanzania wakipata ushindi mara moja

Bao pekee la JKT Tanzania katika mchezo huo lilifungwa na kiungo mshambuliaji, Daniel Mecha katika dakika ya tano ya mchezo akimalizia kwa kichwa mpira mrefu uliorushwa na mlinzi wa kulia wa timu hiyo, Michael Aidan.

Matokeo hayo yameifanya JKT Tanzania ifikishe pointi 30 ipande kwenye msimamo hadi nafasi ya 14 na kuishusha Ihefu kutokana na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Wakati JKT Tanzania wakipanda kwa nafasi tatu, mambo yameendelea kuwaendea kombo Namungo FC, ambao baada ya kichapo hicho wameendelea kusalia katika nafasi ya 12 wakiwa wamejikusanyia pointi 31 baada ya michezo 23.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/15eddd87308e417588de680faa7cd665.jpeg

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi