loader
Dstv Habarileo  Mobile
Profesa Jay: Muziki wetu umekua

Profesa Jay: Muziki wetu umekua

GWIJI wa muziki wa Bongo Fleva na Mbunge wa zamani wa Mikumi, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ amesema kitendo cha wasanii wengi wa hapa nchini kwenda nje ya nchi kuandaa albamu pamoja na EP ni dalili kuwa muziki wa Tanzania umepiga hatua.

Profesa Jay hivi sasa amerudi kwa kasi katika muziki wa Bongo Fleva akitamba na kibao chake kipya cha ‘Utaniambia Nini’ ambacho kinafanya vizuri katika chati mbalimbali za vituo vya radio na televisheni hapa nchini na nje ya nchi.

Akizungumza na gazeti hili, Profesa Jay alisema muziki ni biashara ambayo inahitaji uwekezaji wa hali ya juu.

“Ukiona vijana jinsi wanavyopambana kuachia nyimbo nzuri ni ishara tosha kuwa sasa muziki wetu unakua.”

“Ukiona jinsi vijana walivyo na morali ya kufanya kazi inafurahisha sana, naamini wamepania kuufikisha mbali muziki wetu,” alisema Profesa Jay.

Alisema anafurahia mapokeo ya wimbo wake mpya wa Utaniambia Nini, jambo linalompa morali wa kuachia nyimbo mpya ili kutowapumzisha mashabiki wake.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a08bcaee06af1afd8e0d3c0d702b0614.jpeg

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi