loader
Dstv Habarileo  Mobile
Machinga lipieni vitambulisho, dumisheni usafi

Machinga lipieni vitambulisho, dumisheni usafi

MAENEO mengi hapa nchini hususani mijini kuna wafanyabiashara wadogo maarufu Wamachinga ambao hujihusisha na shughuli za mbalimbali za kibiashara hasa uuzaji wa bidhaa za kati na chini.

Machinga hawa huuza bidhaa kwa bei rahisi hivyo kuwavutia zaidi wateja kipato cha kati na chini.

Ruhusa ya kuuza bidhaa hizo mahala popote ilitolewa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Magufuli ambaye aliwataka kuwa huru kuuza bidhaa mahala popote nchini ili mradi wanunue kitambulisho cha mjasiriamali maarufu kama kitambulisho cha Mmachinga kinachotolewa kwa Sh 20,000.

Kitambulisho hicho kimekuwa kikinunuliwa kupitia halmashauri lakini kwa sasa wigo umeongezwa zaidi ambapo Wamachinga wanaweza kukipata kupitia njia ya kidigitali kama vile kupitia duka mtandao la Machinga App au tovuti ya Tamisemi.

Hakika, kuongezwa kwa njia hizi mbili za kulipia kumelenga kuimarisha ulipwaji wa haraka wa vitambulisho hivyo, hivyo Mmachinga anaweza kwenda halmashauri akanunua au kupitia njia hizo za kidigitali.

Hivyo wamachinga wanapaswa kuvilipia kwa wakati vitambulisho hivyo ili kutoa mchango wao katika ukuzaji wa uchumi wa nchi unapatikana.

Wamachinga ni vema mkakumbuka hali ilivyokuwa kabla ya kupatiwa ruhusa ya kufanya biashara kila sehemu muitakayo, mlikuwa mkifanya biashara katika mazingira ya wasiwasi muda wote, hivyo kwa kuwezeshwa kufanya biashara mahala popote ni thamani mliyopewa ambayo mnatakiwa kuienzi.

Aidha, napenda kuwakumbusha kuzingatia usafi katika mazingira mnayofanyia biashara, mfano katika maeneo ya katikati ya jiji la Dar es Salaam siyo jambo la kushangaza kukuta Wamachinga wakifanya biashara katika mazingira yaliyokithiri uchafu.

Uchafu huu siyo tu kutokana na utitiri wa mabanda ya kufanyia biashara, ila kuna baadhi ya Wamachinga kwao usafi siyo kipaumbele, utakuta mahala wanapofanyia biashara pachafu hadi kero.

Wapo Wamachinga wanaouza bidhaa za vyakula maarufu Mama Lishe ambao huuza vyakula kama wali, ugali na mboga nyingine wakiosha vyombo hawana mahala pa kumwaga maji yenye mabaki ya vyakula na kuishia kuyamwaga hovyo mtaani, hapo ndipo suala la uchafu huibuka.

Sina maana ya kuwa ninakejeli ruhusa hiyo iliyotolewa kwao ya kufanya biashara sehemu mbalimbali za mijini, ila ninawakumbusha kuwa kama wakiendekeza uchafu watageuka kuwa kero.

Ninasisitiza kuwa, Wamachinga mnalo jukumu la kulipia vitambulisho vya ujasiriamali na pia kuimarisha usafi wa maeneo mnayofanyia kazi ili kuondoa uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko na pia kupendezesha mazingira ya biashara zenu.

Ni imani yangu kuwa uongozi wa Jiji la Dar es Salaam ambapo maeneo mengi ya katikati ya jiji yapo wilaya ya Ilala, ni imani yangu kuwa uongozi wa jiji pia utasisitizia usafi kwa Wamachinga hao.

Uuzwaji wa vyakula kwa Mamalishe hasa katika maeneo ya mijini ni lazima uangaliwe kwa jicho la pili hasa katika uzingatiaji wa usafi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6160e9b3dc7d426354790cccbac6870a.jpeg

LIGI Kuu ya Tanzania inaelekea ukingoni ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi